Dar es Salaam. Maombi ya ridhaa ya kufungua shauri kupinga kuvuliwa uanachama ya wabunge 19 wa viti maalum akiwamo Halima Mdee na wenzake yatasikilizwa leoJuni 30, 2022.
Mahakama Kuu imepanga kusikiliza maombi hayo leo baada ya Chadema kuondoa pingamizi lake dhidi ya maombi yao ya zuio la muda (kulinda ubunge wao) hadi maombi yao ya ridhaa yaamuriwe.
Pia kina Mdee wameondoa pingamizi lao dhidi ya kiapo kinzani cha Chadema.
Akiomba kuondoa pingamizi hilo, kiongozi wa jopo la mawakili wa Chadema, Peter Kibatala ameieleza Mahakama jana Jumatano Juni 29,2022 kuwa hawana nia tena ya kupinga amri ya zuio kwa kuwa amri hiyo ni hiyari ya mahakama.
Hivyo Jaji Mustapha Ismail ametoa amri rasmi ya zuio la muda dhidi ya hatua yoyote inayoweza kuwasababisha kina Mdee kuvuliwa ubunge, hadi maombi yao ya msingi ya ridhaa ya kufungua shauri rasmi la kupinga kuvuliwa uanachama yatakapoamuriwa.