CAG Kichere naye alia na Tume ya uchaguzi ifumuliwe

Dar es Salaam. Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG), Charles Kichere ameishauri Serikali kuipa nguvu Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) kuajiri watumishi wake watakaoweza kusimamia uchaguzi kwa haki badala ya kuendelea kutegemea waliopo kwenye mfumo wa Serikali.

Mei 10, 2019, Mahakama Kuu ilitoa hukumu ya kubatilisha vifungu vya 7(1) na 7(3) vya sheria ya uchaguzi vinavyowapa mamlaka wakurugenzi wa miji, wilaya, manispaa na majiji kuwa wasimamizi wa uchaguzi kwenye maeneo yao.

Shauri hilo lilifunguliwa na mwanaharakati wa Katiba, Bob Wangwe akishirikiana na Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC).

Hata hivyo, Serikali ilikata rufaa kuipinga hukumu huyo na baadaye Oktoba 2019 Mahakama ya Rufani ikabatilisha uamuzi na hivyo kuruhusu wakurugenzi waendelee kusimamia uchaguzi.

Pamoja na uamuzi huo, suala hilo limeendelea kulalamikiwa na na sasa limeibuka mara kadhaa wakati wa kutoa maoni katika kikosi kazi kilichoundwa na Rais Samia Suluhu Hassan kuhusu demokrasia ya vyama vingi vya siasa.

Miongoni mwa waliozungumzia suala hilo ni CAG Kichere, ambaye ameungana na viongozi wengine kupendekeza uwepo muundo wa tume ya uchaguzi utakaoifanya iwe huru na hivyo kuaminika zaidi.

Previous Post
Next Post

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *