Saudi Arabia yafungua anga zake kwa ndege za utawala wa Kizayuni

Vyanzo vya habari viliripoti Leo hii asubuhi kwamba Saudi Arabia imefungua anga zake kwa njia zote za usafiri wa anga.

Vyanzo hivyo vimeripoti kuwa Saudi Arabia imefungua anga yake kwa njia zote za usafiri wa anga zinazozingatia kanuni za anga za nchi hiyo.

Kwa mujibu wa ripoti ya Reuters, Kurugenzi Kuu ya Usafiri wa Anga ya Saudi Arabia ilitangaza kuwa Riyadh ilichukua uamuzi huo ili kukamilisha hatua zinazohitajika ili kuimarisha nafasi ya Saudi Arabia kama kitovu cha kimataifa kinachounganisha mabara matatu na kuimarisha mawasiliano ya anga ya kimataifa.

Moja ya matokeo muhimu zaidi ya uamuzi huu ni kwamba kuanzia sasa ndege za utawala wa Kizayuni zitaruhusiwa kutumia anga ya Saudi Arabia kuruka kuelekea India na China.

Hatua hiyo ya Saudi Arabia ilichukuliwa saa kadhaa baada ya tovuti ya Axios kuripoti kuwa utawala wa Kizayuni umeafiki mpango wa jumla kuhusu hadhi ya kisheria ya visiwa viwili vya Misri katika Mlango wa bahari wa Tiran siku ya Alhamisi. Hatua hii inafungua njia ya kuhalalisha uhusiano kati ya Riyadh na Tel Aviv.

Tovuti ya Axios iliandika kwamba makubaliano hayo, ambayo yamejadiliwa kwa siri kwa miezi kadhaa, yatakuwa mafanikio muhimu ya sera ya kigeni kwa utawala wa Joe Biden katika eneo la Asia Magharibi.

Kwa mujibu wa makubaliano ya Camp David kati ya Misri na Israel, Misri imejitolea kuzipokonya silaha Tiran na Sanafir na kukubaliana na ombi la Tel Aviv la kutumwa waangalizi wa kimataifa chini ya amri ya Marekani katika visiwa hivi.

Saudi Arabia ilikabidhi udhibiti wa visiwa hivi viwili, ambavyo ni lango la bandari za Aqaba na Eilat, kwa Misri mwaka 1950. Sasa mashauriano ya pande tatu yanaendelea ili kurudisha umiliki wa visiwa hivi kwa Saudi Arabia.

Licha ya maandamano ya umma nchini Misri, bunge la nchi hiyo mwezi Juni 2017 na Mahakama ya Juu ya Misri mwezi Machi 2018 ziliidhinisha makubaliano ya kuhamisha umiliki na mamlaka ya visiwa hivi viwili hadi Saudi Arabia; Lakini makubaliano haya pia yalihitaji ridhaa na idhini ya utawala wa Kizayuni kutokana na mapatano ya mwaka 1979.

Previous Post
Next Post

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *