Mkutano wa Jeddah ni mchanganyiko kati ya utawala wa Marekani na uhalalishaji wa Waarabu

Mtu fulani alisema kuhusu mkutano wa Jeddah: Waarabu hawakuunganishwa na udugu wao, dini yao, Uarabu wao, utamaduni wao, historia yao, jiografia, kushindwa au kukatishwa tamaa, lakini Biden aliwaleta pamoja nchini Saudia.

Kila mmoja wa viongozi wa Kiarabu aliyekutana na Rais wa Marekani Joe Biden leo hii katika mji wa Jeddah wa Saudi Arabia aliwasilisha malengo ya kuhalalisha uwepo wao katika mkutano huu, japo malengo hayo yote yalikuwa yanakinzana kabisa na lengo la Marekani la kuijumuisha Israel katika mhimili mpya dhidi ya Iran.

Sawa na viongozi wengine wa nchi za Kiarabu, Biden hakupoteza muda wa mkutano huo katika kushughulikia masuala yasiyo muhimu ili kuficha lengo halisi la mkutano huo na mara moja aliingia katika suala kuu na kuwaambia viongozi wa Baraza la Ushirikiano la Ghuba ya Uajemi, Iraq, Jordan na Misri: Tutaimarisha ulinzi wetu wa anga na mfumo wa tahadhari za mapema ili kukabiliana na vitisho vya angani, na kamwe hatutaruhusu Iran kupata silaha ya nyuklia, na hatutaacha ombwe lolote katika eneo hilo kwa manufaa ya Urusi, China na Iran.

Inaonekana Biden alifurahishwa na uungwaji mkono wa viongozi wa Kiarabu kwa malengo yake, lakini alifurahishwa zaidi na maneno ya Mohammed bin Salman, Mrithi wa Kifalme wa Saudia aliposema kwamba Saudi Arabia itaongeza uwezo wake wa uzalishaji wa mafuta hadi mapipa milioni 13 kwa siku.

Makusudio ya safari ya Biden katika eneo na kukutana kwake na viongozi wa nchi za Kiarabu yalikua ni mafuta ya Saudia na usalama wa utawala wa Kizayuni, hata kama atautoa muhanga usalama wa nchi za Kiarabu na kuzilazimisha kuingilia katika vita dhidi ya nchi zinazoipinga Marekani. .

Lakini katika mandhari haya yenye kufedhehesha ya Waarabu, sauti ya adhama na heshima ya Kiislamu ilisikika kutoka kwa watu wa Yemen, ambapo Muhammad Ali Al-Houthi, mjumbe wa Baraza Kuu la Kisiasa la Yemen, alisema kwamba uamuzi wowote waweza fanyika, lakini uamuzi uko mikononi mwenu na mnaifahamu hili.

Kwa kusema hivyo, alithibitisha kwamba watu wa Yemen hawajatilia maanani chochote kwa Amerika na Biden, hawaombi kukutana na Wamarekani, wanadai amani ya kweli huko Yemen na kusimamishwa kwa uchokozi na mzingiro kutoka pande zote, na vilevile usaliti wa Biden kutoka Saudi Arabia kuanzisha utawala pasi na kujali eneo ambalo utawala wa Kizayuni uko juu ya piramidi.

Previous Post
Next Post

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *