Kikosi cha Ulinzi wa Anga cha Jeshi la Syria kimetangaza kutungua makombora yaliyokuwa yamevurumishwa na utawala haramu wa Israel nje ya mji mkuu Damascus.
Shirika rasmi la habari la Syria, SANA limetangaza kuwa, mizinga ya ulinzi wa anga ya Syria alfajiri ya leo Ijumaa imetungua akthari ya makombora hayo ya Israel viungani mwa Damascus.
Jeshi katili la Israel limelenga maeneo kadhaa ya Damascus katika chokochoko hizo mpya, ingawaje maeneo yaliyolengwa hayajabainika.
Hata hivyo sauti kubwa za miripuko zimesikika katika maeneo ya Al-Sidiyah Zainab na Qudsayya, nje kidogo ya mji mkuu wa nchi hiyo ya Kiarabu.
Habari zaidi zinasema kuwa, wanajeshi watatu wa Syria wameuawa shahidi kwenye shambulio hilo la makombora ya Wazayuni, huku wengine saba wakijeruhiwa.
Utawala haramu wa Israel ni muungaji mkono mkubwa wa magaidi ambao wanataka kuiangusha serikali halali ya Rais Bashar al Assad nchini Syria.