Hotuba ya Ijumaa – 29 Julai 2022, Hujjatul Islam Ustad Syed Jawad Naqvi

Hotuba ya Ijumaa – 29 Julai 2022

 Hujjatul Islam Ustad Syed Jawad Naqvi

 (Mkuu wa shule Jamia Orwatul Wuthqa – Lahore)

 Imetolewa: Msikiti wa Baitul Ateeq

 Lahore – Pakistan

Khutba ya 1: Msingi wa kila tendo la kidini ni Taqwa

Ninawausieni nyinyi pamoja na kuiusia nafsi yangu kumcha Mwenyezi Mungu, na nawasisitizieni kuyasimamisha maisha yenu katika misingi ya Uchaji Mungu (Taqwa).Taqwa ni mjumuiko wa mipango na mikakati kutoka kwa Mwenyezi Mungu yenye kumlinda mwanadamu. Mikakati anayopaswa kutekeleza katika maisha yake ili apate kufanikiwa.

Mfano wa maisha yasiyo na Taqwa ni kama yale wanayoyapitia kizazi cha sasa na Waislamu wanateseka kwa sababu ya kukosa Taqwa katika maisha yao. Majanga wanayoyapata Waislamu kwa kukosa Taqwa yanatosha kuwa funzo kwetu sisi ambapo tunaweza kumuona mwanadamu anaishi maisha kama mnyama pasi na kuzingatia misingi ya Taqwa na kupelekea maisha yake kuwa magumu.

Kati ya mambo yaliyozungumziwa zaidi na Mwenyezi katika Quran ni yale yenye mafungamano na Taqwa. Taqwa imetajwa moja kwa moja katika Suratul Baqarah aya ya 203 ambapo aya hizi zinahusiana na ibada ya Hija.

وَاذْكُرُوا اللَّهَ فِي أَيَّامٍ مَعْدُودَاتٍ ۚ فَمَنْ تَعَجَّلَ فِي يَوْمَيْنِ فَلَا إِثْمَ عَلَيْهِ وَمَنْ تَأَخَّرَ فَلَا إِثْمَ عَلَيْهِ ۚ لِمَنِ اتَّقَىٰ ۗ وَاتَّقُوا اللَّهَ وَاعْلَمُوا أَنَّكُمْ إِلَيْهِ تُحْشَرُونَ

Na mtajeni Mwenyezi Mungu katika zile siku zinazo hisabiwa. Lakini mwenye kufanya haraka katika siku mbili (akarejea) si dhambi juu yake; na mwenye kukawia pia si dhambi juu yake, kwa mwenye kumchamngu.

Na mcheni Mwenyezi Mungu, na jueni kwamba nyinyi mtakusanywa kwake.

Vilevile kabla ya Aya hizi kuna utajo unaohusiana na Taqwa pekee.

Katika aya nambari 197 imetajwa kuwa

الْحَجُّ أَشْهُرٌ مَعْلُومَاتٌ ۚ فَمَنْ فَرَضَ فِيهِنَّ الْحَجَّ فَلَا رَفَثَ وَلَا فُسُوقَ وَلَا جِدَالَ فِي الْحَجِّ ۗ وَمَا تَفْعَلُوا مِنْ خَيْرٍ يَعْلَمْهُ اللَّهُ ۗ وَتَزَوَّدُوا فَإِنَّ خَيْرَ الزَّادِ التَّقْوَىٰ ۚ وَاتَّقُونِ يَا أُولِي الْأَلْبَابِ

Hija ni miezi maalumu. Na anaye kusudia kufanya Hija katika miezi hiyo, basi asiseme maneno machafu wala asifanye vitendo vichafu wala asibishane katika Hija. Na kheri yoyote mnayo ifanya Mwenyezi Mungu anaijua.

Na jitengezeeni zawadi. Na hakika bora ya zawadi ni uchamngu. Na nicheni Mimi, enyi wenye akili!

Aya inaamrisha kuwa Hija ifanyike katika miezi maalumu tu na mambo mengi ambayo yanaruhusiwa kabla ya Hija yaharamishwe wakati wa hija.

Katika aya hii, Taqwa inahesabiwa kuwa ni ‘Zaad’ ambayo ni  mahitaji muhimu aliyonayo msafiri wakati wa safari kama vile chakula, mavazi na usafiri. Katika Hija unazuru kwa madhumuni makubwa na kwa ajili hiyo unahitaji hazina itakayoweza kukidhi mahitaji yako.

Kati ya mahitaji hayo ni yale yanayokufanya uweze kufika katika mji wa Makka kama vile chakula, tikiti ya ndege, pesa n.k. lakini kuna riziki nyingine inayokufanya ufikie malengo ambayo ni Taqwa.

Hapa Taqwa haina maana ya  kujiepusha tena ambapo mwanadamu anajiepusha na Haramu fulani, bali maana yake ni mtu  kuchukua hatua za usalama kwa ajili ya nafsi yake iliaweze kufikia lengo la Hija. Kwa kua Hija haifanywi pasi na mafunzo na elimu. Kama ambavyo Imam Sajjad (a.s) alivyomueleza Shibli kwamba ingawa umefuata taratibu zote za dhahiri za Hija lakini bado hujahiji na kwamba hujafanya kitu.

Hakua ameacha hukumu yeyote kwa mujibu wa Fiqh na sheria na kisha akafanya ibada zote kwa usahihi lakini bado Imam akuamuambia kua hajahiji.  Vilevile leo hii watu wanatembelea Makka lakini hawafanyi Hija. Kwa sababu kati ya masharti muhimu ya Hajj ni Taqwa na vilevile kuna masharti ya Taqwa ambayo ni muhimu katika Hija.

Riziki hii sio mahususi kwa ajili ya Hijja tu kwa sababu hizi ni riziki za maisha na hivyo makusudio ya Hija, maisha na uumbaji hupatikana katika riziki hii ya Taqwa. Na Taqwa maana yake ni ulinzi na zile hatua zote za usalama, mipango, mambo yote aliyoyataja Mwenyezi Mungu Lau yatafanyiwa kazi na mwanadamu, anakuwa salama na anaweza kufikia lengo la Hija na maisha kiujumla.

Yule ambaye hayuko salama ni yule aliyemateka wa matamanio yake, shahawa, Shetani na maisha ya kimaada, kiongozi ni mtu asiyejiamini na asiyekuwa na utulivu, hawezi kufikia lengo la Hija.

Kisha maana zile zile zinaendelea hadi Aya ya 203

وَاذْكُرُوا اللَّهَ فِي أَيَّامٍ مَعْدُودَاتٍ ۚ فَمَنْ تَعَجَّلَ فِي يَوْمَيْنِ فَلَا إِثْمَ عَلَيْهِ وَمَنْ تَأَخَّرَ فَلَا إِثْمَ عَلَيْهِ ۚ لِمَنِ اتَّقَىٰ ۗ وَاتَّقُوا اللَّهَ وَاعْلَمُوا أَنَّكُمْ إِلَيْهِ  تُحْشَرُونَ

Na mtajeni Mwenyezi Mungu katika zile siku zinazo hisabiwa. Lakini mwenye kufanya haraka katika siku mbili (akarejea) si dhambi juu yake; na mwenye kukawia pia si dhambi juu yake, kwa mwenye kumchamngu. Na mcheni Mwenyezi Mungu, na jueni kwamba nyinyi mtakusanywa kwake.

Hapa imetajwa mkumbukeni Mwenyezi Mungu katika zile siku mlizoandikiwa. Nazo ni katika mwezi wa Dhul-hijja tarehe ya 10, 11 na 12. Mwenye kutumia japo siku mbili tu yaani tarehe 11 na 12 na akarudi hakuna lawama na mwenye kutumia siku moja ya ziada; wote wawili niwenye kumcha Mwenyezi Mungu. Nayo aya inaamrisha kumcha mwenyezi Mungu kwa sababu kwake yeye inahisabiwa.

Mwanzo ni kuwa Hija inaanzia tarehe 8 Dhulhijja, ambapo siku ya 9 ni siku ya Arafah kisha usiku wa tarehe 9 anakaa Mashar na baada ya kuchomoza jua wanaruhusiwa kufika Mina. Na kisha watafanya ibada tofautitofauti wakiwa hapo kama vile kutoa dhabihu, kunyoa nywele, kumpiga mawe Shetani na kisha baada ya kuvua Ihram mwenye kuhiji atakaa huko kwa siku mbili zaidi.

Vilevile kuna ruhusa ya  kukaa kwa siku moja zaidi huko Mina ambayo ni Hajj ya 13, ambapo anaweza kufanya dhikr (utajo) wa Mwenyezi Mungu. Utajo huo mahususi ambao ni dhikr na tasbihi ya Idi ambayo inapaswa kusomwa katika sala 10 baada ya siku ya Idi kwa mfululizo kwa mara 10 katika kila Swala. Kisha kuna utaratibu ukiwa Mina wakuweza kupata Taqwa.

Sisi hufikiri kwamba kwa kwenda Hija tunapata Ucha Mungu ambapo tunaichukulia kuwa ni kituo maalum cha kiroho . Kwa mujibu wa Quran Hija hukamilika punde  tu Taqwa inapopatikana.

Katika Suratul Baqarah mwanzoni yenyewe imetajwa kwamba Quran ni muongozo kwa Muttaqeen ( wanaomcha Mwenyezi Mungu) ambao ni wale walio na imani, wanaoswali, na wanafanya Infaq na wanaoiamini siku ya mwisho.

Hapa inatajwa kuwa Muttaqi (mwenye kumcha mwenyezi Mungu) ni yule ambaye atayatekeleza mambo hayo na sio kwamba mwenye kufanya hayo yote anakuwa Muttaqi. Hii ina maana ya kwamba imani ni matokeo ya Taqwa. Kisha Swala, Infaq zote ni natija ya Taqwa.

Katika aya hii ya 203, Mwenyezi Mungu anasema kua unapoipata Taqwa basi Hija yako itakuwa imekamilika, ambapo tunafikiri kwamba kwa kwenda Hija tunakuwa miongoni mwa Muttaqin.

Ukweli wa Taqwa ambayo Quran imeitaja kubwa ndio misingi ya dini. Quran inasema kama wewe ni Muttaqi basi utatekeleza ibada hizi zote ambazo miongoni mwao ni Hija.

وَمِنَ النَّاسِ مَنْ يُعْجِبُكَ قَوْلُهُ فِي الْحَيَاةِ الدُّنْيَا وَيُشْهِدُ اللَّهَ عَلَىٰ مَا فِي قَلْبِهِ وَهُوَ أَلَدُّ الْخِصَامِ

Na katika watu yupo yule ambaye maneno yake kwa maisha ya kidunia hukufurahisha; naye humshuhudisha Mwenyezi Mungu kwa yaliyomo moyoni mwake, na hali yeye ndiye mkubwa wa ukhasimu.

وَإِذَا تَوَلَّىٰ سَعَىٰ فِي الْأَرْضِ لِيُفْسِدَ فِيهَا وَيُهْلِكَ الْحَرْثَ وَالنَّسْلَ ۗ وَاللَّهُ لَا يُحِبُّ الْفَسَادَ

Na anapo tawala hufanya juhudi katika nchi kwa kufisidi humo na kuteketeza mimea na viumbe. Na Mwenyezi Mungu hapendi ufisadi.

وَإِذَا قِيلَ لَهُ اتَّقِ اللَّهَ أَخَذَتْهُ الْعِزَّةُ بِالْإِثْمِ ۚ فَحَسْبُهُ جَهَنَّمُ ۚ وَلَبِئْسَ الْمِهَادُ

Na akiambiwa: Mwogope Mwenyezi Mungu, hupandwa na mori wa kutenda madhambi. Basi huyo inamtosha Jahannam. Paovu mno hapo kwa mapumziko.

Aya hii ya 206 inahusiana na Hadithi ya Imamu Sajjad ambayo tumeijadili hapo mwanzoni ambapo Imam ametutaka tujiepushe na wale wanaofuata uongozi na umaarufu kwakua wataiangamiza dini yetu.

Aya hii inasema kwamba dalili ya mtu mwenye majivuno, anayependwa na watu wengi ni kwamba anapoombwa kumcha mwenyezi Mungu hisia za uwongo na utu wa jinai huingia kati.

Anahisi kwamba umeikanyaga heshima yake kwa kumuamrisha kumcha mwenyezi Mungu. Watu hawa wanapopewa jukumu la kuwa viongozi ardhini wao huiharibu, na Mwenyezi Mungu hawapendi mafisadi.

Watu wa namna hii wanapoelezwa kua unaharibu nchi anahisi ni kana kwamba utu wake unakosolewa au kutukanwa. Izzat ni nguvu inayotukinga kutokana na athari zinazotoka kwa mtu mwingine. Kama ambavyo leo hii mtu anapotunong’oneza tunadanganyika na maneno yake

, Tunaona ni jinsi gani jamii ya Wapakistani inavyokubali kwa urahisi propaganda za vyombo vya habari, uwongo wa wanasiasa, mikanganyiko ya mamufti (wasomi) na ulaghai wa wafanyabiashara.

 Mtu ambaye anaathirika na nguvu za mtu mwengine, ina maana ya kwamba yeye ni mwepesi sana kiasi kwamba anaathirika kutokana na kila kitu. Kwa lugha ya kiarabu anafahamika kama  ‘Dhalil (Zalil)’.

Mtu huyu kutokana na ukosefu wa  Izzat ndani yake na  ustahimilivu unaomkinga kutokana na madhara, Iwapo atatishiwa na mtu akaogopa basi atakua ni Zalil, maana yake ni mtu ambaye ni dhaifu kiasi kwamba kutokana na udhaifu huo amekuwa laini kiasi kwamba anapata athari kutoka kwa kila kitu.

Tunaweza kujitathmini kama tunahesabiwa miongoni mwa Aziz ( mwenye nguvu) au Zalil (asiyena nguvu). Tunapokubali propaganda za uongo basi tunakua Zalil lakini tukipinga na kusimama dhidi ya uongo ule tutakua Aziz au wenye Izzat, Wakati fulani shauku, hisia na hali humzidi mwanadamu.

Aziz ni yule ambaye haathiriki lakini anaikubali Haki na hadhihirishi msimamo mkali dhidi ya ukweli. Ikiwa unaonyesha ugumu dhidi ya ukweli basi wewe ni mkaidi (Ladood).

Kuna baadhi ya watu ni wakaidi kiasi kwamba hawakubali ukweli. Kuna baadhi ya watu ambao mwili wao ni Zalil na ni dhaifu dhidi ya magonjwa na huathirika kwa urahisi mno.. Kuna wengine wana nguvu za mwili ambao hawaathiriwi na magonjwa lakini wanaweza kuwa dhaifu kimwili.

Ni kosa kuonesha ugumu na ukaidi dhidi ya Taqwa. Inatokea pale mtu anapofanya makosa na mtu akamfanyia Amr Bil Maroof (kuamrisha mema) , inamuumiza na haipendi.

Hiki ndicho kitambulisho cha Izzat na Zillah. Ikiwa Amr Bil Maroof (kuamrisha mema) ni wajibu juu yetu na tukachukia basi sisi ni Zalil, lakini tukikubali mawaidha basi sisi ni Aziz. Quran inasema anapata ukaidi wa kuhalifu.

Onyesha ulaini dhidi ya taqwa na ukubali. Iwapo mtu atatoa ombi la moja kwa moja ya kwamba watu wawe na Taqwa au akatoa pendekezo kuhusu baadhi ya marejeo ya lengo la Taqwa kama vile ombi la kuswali Ijumaa.

Natoa mfano tu wa swalah ya ijumaa lakini mambo mengine pia ni hivi. Kwa njia hii Quran inatuongoza kuifanya Taqwa kuwa msingi katika kila sehemu ya maisha.

Mwongozo wa Qur’an ni wa kijamii na maisha ya mtu binafsi yapo kwenye miinuko ya maisha ya kijamii. Maamrisho yote yaliyomo ndani ya Tauzeehul Masael ni ya mtu binafsi, kitendo kimoja cha kijamii kwa ajili ya Swalah ya Ijumaa kipo ambacho pia kimefanywa kuwa sio wajibu. Leo hii wale ambao wana fikra za kibinafsi nao pia wako katika muktadha wa jamii.

Leo hii hatuoni kua wasomi wako pamoja na wanasiasa au kuna njia nyingine ?  Wanazuoni hawa ni waumini wanaofuata sheria za kibinafsi na wakati haujayakubali maisha ya kijamii kulingana na semi za Quran basi utaingia katika maisha ya kijamii ambayo ni ya kishetani. Lau tutaanza na maisha ya kijamii basi tutaingia ndani ya muktadha wa Quran.

Wakati Quran inaamrisha Taqwa inabidi tuikubali na tusiwe wakaidi. Quran inaorodhesha mambo yote ambayo yanafaa kuorodheshwa  chini ya taqwa kama vile Hija . Taqwa inayopatikana wakati wa kuhiji ni daraja moja na ile unayoipata kutoka katika Hija ni daraja nyingine. Hijja hufanywa na yule ambaye amejikinga na Taqwa.

Mtume anasema zitakuja zama ambazo kutakuwa na aina tatu za Hija katika Ummah wangu; moja ilikuwa ya biashara, moja ya safari za kitalii na nyingine ili kupata umaarufu wa kuitwa Hajji au hujaji. Hizi ni Hijja za Wasiokuwa Muttaqin. Mwenye kwenda Hijja kwa Taqwa anafanikiwa kuiga tabia ya Ibrahim.

Katika dini taqwa ni sifa, na uwezo unaoegemezwa juu yake mwanadamu ili aweze kupata daraja fulani. Mwenye sifa anapoingia kwenye dini basi anapata daraja moja baada ya nyingine katika dini. Uwezo huu unampeleka mwanadamu kwenye Hija.

Iwapo Hija ni kama ile ya Ibrahim a.s na akawa sehemu ya Msafara fulani basi Msafara huo unaweka kuwa na shinikizo aina zote za kumtoa kwenye Hija kama ya Nabii  Ibrahim na kumfanya ahiji hija ya kitalii.

Maulana anazo Fatwa zote zenye kumtoa kutoka katika hija kama ile ya Nabii Ibrahim a.s.

Hija ya Nabii Ibrahim a.s inaanza kuanzia tarehe 9 Dhulhijja na kutoka kwenye Ba’raat ni kujitenga. Unaweza kutembea na misafara yote na yote ikakupa Fatwa kwamba usifanye Ba’raat.

Ikiwa mtu ni Muttaqi basi atafanya Hija kama ile ya Nabii Ibrahim, na atakaporudi baada ya hapo atakuwa na uwezo wa juu na utofauti wa taqwa.

Alivyokwenda Hija alikua ni mtu Muttaqi na alikua na mfano wa mtu wa kawaida lakini anaporudi, anakua kama Nabii Ibrahim ambaye ni mvunja masanamu, yupo tayari kutoa kila kitu katika njia ya Mwenyezi Mungu.

Taqwa ile ya mwanzo imemfanya afikie daraja hiyo na kisha akarejea na haiba ya nabii Ibrahim a.s na hivi sasa atafanya hivyo katika jamii yake kama alivyofanya nabii Ibrahim.

Ikiwa Taqwa hii itakuwa ndio msingi wa kila kitu kama vile mfumo wa elimu, Msikiti, siasa, biashara basi matokeo yale yale ya Taqwa yatatoka ambayo Quran imetaja kwa Ibrahimi Hajj.

Khutba ya 2: Moyo ni hifadhi ya Hekima

Kwa kusema no 108

 وَ قَالَ عليه السلام: لَقَدْ عُلِّقَ بِنِيَاطِ هَذَا الْإِنْسَانِ بَضْعَةٌ هِيَ أَعْجَبُ مَا فِيهِ وَ ذَلِكَ الْقَلْبُ وَ ذَلِكَ أَنَّ لَهُ مَوَادَّ مِنَ الْحِكْمَةِ وَ أَضْدَاداً مِنْ خِلَافِهَا فَإِنْ سَنَحَ لَهُ الرَّجَاءُ أَذَلَّهُ الطَّمَعُ وَ إِنْ هَاجَ بِهِ الطَّمَعُ أَهْلَكَهُ الْحِرْصُ وَ إِنْ مَلَكَهُ الْيَأْسُ قَتَلَهُ الْأَسَفُ وَ إِنْ عَرَضَ لَهُ الْغَضَبُ اشْتَدَّ بِهِ الْغَيْظُ وَ إِنْ أَسْعَدَهُ الرِّضَى نَسِيَ التَّحَفُّظَ وَ إِنْ غَالَهُ الْخَوْفُ شَغَلَهُ الْحَذَرُ وَ إِنِ اتَّسَعَ لَهُ الْأَمْرُ اسْتَلَبَتْهُ الْغِرَّةُ وَ إِنْ أَفَادَ مَالًا أَطْغَاهُ الْغِنَى وَ إِنْ أَصَابَتْهُ مُصِيبَةٌ فَضَحَهُ الْجَزَعُ وَ إِنْ عَضَّتْهُ الْفَاقَةُ شَغَلَهُ الْبَلَاءُ وَ إِنْ جَهَدَهُ الْجُوعُ قَعَدَ بِهِ الضَّعْفُ وَ إِنْ أَفْرَطَ بِهِ الشِّبَعُ كَظَّتْهُ الْبِطْنَةُ فَكُلُّ تَقْصِيرٍ بِهِ مُضِرٌّ وَ كُلَّتْهُ الْبِطْنَةُ فَكُلُّ تَقْصِيرٍ بِهِ مُضِرٌّ وَ كُلُّ إِلُّ إِفُّدَهُّ ِفْعَلَهُمْ فَكُلُّ

Amirul-mu’minin, amani iwe juu yake, amesema: Ndani mwa mwanadamu mna kipande cha nyama kilichounganishwa kwake na mshipa na ni kitu cha ajabu zaidi kilichomo ndani yake, nacho ni moyo. 

Kina akiba ya hekima na mambo yalio kinyume na hekima.  Kinapoona miale ya matumaini, shauku inakifedhehesha na shauku inapoongezeka, pupa inakiharibu.  Pindi kinapopatwa na tamaa, huzuni huiua.  hasira inapoongezeka ndani yake, ghadhabu kali huipata.  Kinapobarikiwa na raha, kinasahau kuwa mwaangalifu. 

Kinapopatwa na uoga, kinakuwa kisichojali.  Amani ikienea pande zote, kinakuwa chenye kupuuza.  Kinapopata mali, uhuru wa kutohitajia hukiweka katika makosa.  KInapopatwa na Matatizo, ukosefu wa subira hukifanya kuwa kiyenyekevu. 

Kinapokabiliwa na njaa, hupatwa na dhiki ,  Ikiwa njaa itakishambulia, udhaifu hukifanya kikae chini.  Ikiwa kula kwake kunaongezeka, uzito wa tumbo hukiumiza.  Kwa hivyo, kila kichache kina madhara kwake na kila ziada ni madhara kwake.” 

Maana ya kwanza iliyoelezwa ni kwamba mwanadamu ana moyo, kisha moyo huu ambao una hekima pia una hali zake zingine zenye utata. Jambo la tatu ambalo Amirul Momineen (a) anafafanua, ni kwamba hali zinazokuzwa moyoni zina mfumo.

Na kama pia tulivyoelezwa hapo awali kwamba Imamu Sadiq (a) anasema kwamba kuna nguvu ya akili (Aql) na nguvu ya Jahal (upumbavu). Imamu (a) akauliza je unapenda nikijulishe sifa za kikosi cha akili na cha upumbavu?

Tunapata katika hadithi hii, na nyinginezo kuwa sifa hizi zinafungamana kifamilia, ambapo baadhi yake zinatokana na sifa  nyingine zinazotoka kwao au zinahusiana nao.

Tukishaelewa ukweli huu kwamba hakuna sifa iliyo peke yake, msemo tunaosema mfano “mtu huyu anaongea uwongo tu na wala  hatujapata chochote kibaya kwake. Lakini ukweli ni kuwa uwongo haui pekee yake bali kuna seti kamili ya sifa zingine zinazoambatana nayo. Na vile vile sifa nzuri pia zipo kama familia.

Mfano Imam Ali (a) sifa moja inayojulikana kwake ni ujasiri. Lakini ujasiri hauwi pekee yake bali pamoja nayo ni familia kamili. Kama Vile vile dhidi ya ujasiri ni woga (Jubn) lakini ikiwa mtu ni mwoga basi hii sio sifa pekee aliyo nayo. 

Allama Ansari katika kitabu chake anasema kwamba ukikuta sifa moja kwa mtu basi kwa mujibu wa Fiqh unaweza kuhusisha sifa nyingine zinazohusiana na sifa hiyo pia.

Amirul Momineen (a) katika msemo huu anaeleza maana ya tatu kwamba ikiwa sifa moja itakuzwa basi nyingine zinazohusiana nayo zitakuja. Mfano wa kwanza ni سَنَحَ لَهُ الرَّجَاءُ أَذَلَّهُ الطَّمَعُ .

Matumaini yanapojengeka ndani ya mwanadamu jambo la pili linalojitokeza ni shauku, basi shauku inapokuja basi uchoyo huandamana nayo. RAJA (Tumaini)  hutokana na sifa nzuri na dhidi ya yake ni kukata tamaa.

RAJA inamaanisha kuwa na hamu ya kupata kitu ambacho kinaweza kupatikana kwa njia ya kuridhisha. Matarajio ya kupata kitu ambacho upatikanaji wake unawezekana, au una uhakika wa kukipata au kuna alama za kuridhisha kwamba kinaweza kupatikana kwa Kiarabu ni RAJA.

Kama vile ukitarajia mvua katika msimu wa masika, basi inawezekana na angalau unaridhika kuwa mvua itanyesha. Haya ni matumaini (RAJA). Kisha kuna na sifa kinyume chake ambayo ni sifa ya Tamaa, ambayo pia ni matumaini lakini ya kitu ambacho hakiwezi kupatikana kwa kawaida na kwa kweli mwanadamu anakata tamaa ya kukipata. RAJA ni tumaini la kile kinachowezekana, kinachotarajiwa na kilicho karibu na chenye uhakika.

Kisha TAMA ni matamanio ambayo hayatarajiwi kutimizwa, hakuna uhakika na kukata tamaa. Kama vile mwanafunzi amefanya mtihani lakini anakata tamaa ya kufaulu na anahisi hatarajiwi kufaulu mtihani huo. Kisha HIRS pia ni aina ya tamaa bali ni ile tamaa inayomtawala na kumchukua mwanadamu.

Tuna matamanio mengi ambayo yamekandamizwa ndani ya mioyo yetu na sio ya kuambiwa mtu yeyote. HIRS ni ile tamaa ambayo mwanadamu hawezi kuificha na inakuwa inatawala sana moyo, na akili ya mwanadamu.

Tamaa hiyo hata ikiwa tunataka kujificha basi pia hatuwezi kuificha. Kama vile mtu aliye na njaa, au mtu anayetamani tamaa kwa njia ambayo hata akitaka kujificha hawezi.

Amirul Muminin (a) anasema kwamba moyo ni hifadhi ya hekima na mambo yake yenye utata. Kisha kitu kikikua moyoni basi kingine pia kinazalika ambacho ni kikali zaidi kuliko cha kwanza, na kisha cha tatu ambacho kinapozalika basi kinakuwa kikali zaidi kushinda cha pili. Mwanadamu anapokuza tumaini moyoni, basi anakua na hamu  kwa ajili ya kufikia mambo yasiyowezekana na wakati haya yanapojitokeza basi anatawaliwa na matamanio yale ambayo yanamfanya ashindwe kujidhibiti.

Ali (a) anasema wakati wowote ambao mwanadamu anapokuwa na matumaini kamwe hatadhalilishwa, lakini akiwa mwenye TAMA basi tamaa ile itamfedhehesha. Matumaini yanapokua basi endelea na hayo tu. Mtume anasema mimi nina wasiwasi na mambo mawili katika Ummah wangu, moja ni matumaini ya kudumu na la pili ni kufuata matamanio duni.

RAJA (tumaini) ni miongoni mwa sifa chanya kwa sababu kukata tamaa ni sifa mbaya. Pia tunapaswa kuwa na matumaini na tusikate tamaa. Weka matumaini lakini usiruhusu igeuke kuwa tamaa na pupa.

Mwanadamu akikuza Tumaini, basi tamaa inafedhehesha tumaini na jeshi la tamaa linapofanya uchokozi kwa mwanadamu basi pupa itamuangamiza mwanadamu. Matumaini ni sifa chanya, basi shauku ni sifa hasi na tamaa ni hatari zaidi.

Tumaini linapokuja tunahitaji kusawazisha na tusiruhusu kufikia kiwango cha juu. Wale ambao wamejiangamiza wenyewe ni kutokana na hili.

Previous Post
Next Post

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *