Uhusiano wa Uturuki na Israel walipiga jambia kwa nyuma taifa la Palestina

Kiongozi mmoja wa ngazi za juu wa Harakati ya Ukombozi wa Wananchi wa Palestina amelaani vikali hatua ya Uturuki ya kurejesha uhusiano wa kawaida na utawala wa Kizayuni wa Israel.

Jumatano iliyopita, Uturuki na utawala wa Kizayuni zilikubaliana kufufua uhusiano baina yao baada ya kusimama kwa muda wa miaka minne.

Mwaka 2018 Uturuki ilisimamisha uhusiano wake na Israel baada ya wanajeshi wa utawala wa Kizayuni kuwashambulia Wapalestina waliokuwa wanashiriki katika maandamano ya Ghaza ya kupigania kurejea katika ardhi za mababu zao. Wanajeshi makatili wa Israel waliua shahidi na kwa umati makumi ya Wapalestina. Kufuatia jinai hiyo ya Wazayuni, serikali ya Uturuki iliamua kumrejesha nyumbani balozi wake aliyekuweko Tel Aviv. Sasa hivi lakini pande hizo mbili zimeamua kufufua uhusiano wao kana kwamba hakuna jinai yoyote iliyofanywa na wanajeshi Wazayuni dhidi ya Wapalestina wasio na ulinzi.

Ahmad Kharis, mmoja wa viongozi waandamizi wa Harakati ya Ukombozi wa Wananchi wa Palestina sambamba na kulaani hatua ya Uturuki ya kurejesha uhusiano wake na utawala katili wa Kizayuni, ameliambia shirika la habari la Iran Press kuwa, utawala wa Recep Tayyip Erdogan tangu hiyo zamani haukuwa na nia ya kweli ya kulisaidia taifa la Palestina. Hata kitendo cha Erdogan cha kujifanya kulihami taifa la Palestina kilifanyika kwa nia ya kutumia vibaya tu kadhia ya Palestina kwa manufaa yake binafsi na kwa shabaha ya kufanikisha njozi yake ya kurejea kwenye nguvu za Ufalme wa Uthmania (Ottoman Empire) wa Waturuki.

Amesema, tangu huko nyuma, Harakati ya Ukombozi wa Wananchi wa Palestina haikutekwa wala kulaghaiwa na hila hizo za Erdogan na utawala wake.

Previous Post
Next Post

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *