Makumi ya magaidi wakufurishaji waangamizwa nchini Burkina Faso

Jeshi la Burkina Faso limetangaza kuwa, limeangamiza magaidi 100 wakufurishaji katika operesheni za kijeshi lilizofanya kwa nyakati tofauti katika nchi hiyo ya magharibi mwa Afrika.

Shirika la habari la Tasnim limenukuu taarifa ya jeshi la Burkina Faso ikitoa ufafanuzi kwa kusema, operesheni zilizoangamiza magaidi hao 100 wakufurishaji zimefanyika kwenye maeneo mbalimbali na kwa nyakati tofauti nchini humo na zimefanyika katika kipindi cha baina ya tarehe 15 Julai hadi 15 Agosti, 2022.

Katika kipindi cha miaka ya hivi karibuni, magenge ya kigaidi yamefanya mashambulio mengi ya kigaidi katika maeneo tofauti ya Burkina Faso hasa ya kaskazini mwa nchi hiyo. Wimbi la mashambulizi ya magaidi hao lilianzia kaskazini, baadaye yakaenea mashariki na hivi sasa yameshafika hadi katikati ya Burkina Faso.

Burkina Faso inapakana na nchi kama za Niger na Mali ambazo zimejaa magenge ya kigaidi ya ukufurishaji. Tangu mwaka 2015 nchi hiyo imekumbwa na mashambulio ya magenge ambayo yamejitangaza kuwa ni sehemu ya mitandao ya kigaidi ya al Qaida na Daesh yaani ISIS.

Hadi hivi sasa maelfu ya wananchi wa Burkina Faso imma wameuawa au kujeruhiwa na karibu milioni mbili wamelazimika kuyakimbia makazi yao kutokana na kuongezeka sana mashambulizi ya magenge ya kigaidi.

Mara kwa mara kumekuwa kukitokea pia mauahi ya umati nchini Burkian Faso. Mauaji ya karibu kabisa ya umati yaliyolikumba eneo la kaskazini mwa nchi hiyo ni yale yaliyotokea katikati ya mwezi Juni ambapo watu 86 waliuawa kikatili katika uvamizi wa magenge ya kigaidi na ukufurishaji.

Previous Post
Next Post

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *