Wakuu wa nchi tatu za Ulaya, Ufaransa, Ujerumani na Uingereza, walifanya mazungumzo kwa njia ya simu na Biden siku ya Jumapili kuhusu mazungumzo na Iran na usalama wa vinu vya nyuklia vya Ukraine.
Waziri Mkuu wa Uingereza Boris Johnson, Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron, Kansela wa Ujerumani Olaf Schultz na Rais wa Marekani Joe Biden walizungumza kwa njia ya simu Jumapili.
Mojawapo ya mada ya mazungumzo haya ya pamoja ya simu ilikuwa juu ya usalama wa kinu cha nyuklia cha Zaparozhia nchini Ukraine.
Kwa mujibu wa taarifa ya Ikulu ya White House, wakuu wa nchi tatu za Ulaya na Biden katika mazungumzo hayo ya simu pia wamezungumzia mazungumzo ya sasa kuhusu mpango wa nyuklia wa Iran na kusisitiza haja ya kuimarishwa uungaji mkono kwa washirika katika eneo la Mashariki ya Kati na juhudi za pamoja kuzuia na kupunguza Iran.