Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran awasali nchini Mali na kuonana na wenyeji wake

Waziri wa Mambo ya Nje wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran anaendelea na ziara yake ya kuzitembelea nchi za Afrika na tayari ameanza mazungumzo na viongozi wa Mali akiwemo Waziri wa Mambo ya Nje wa nchi hiyo ya magharibi mwa Afrika.

Hossein Amir-Abdollahian ameandamana na ujumbe wa ngazi za juu wa kisiasa na kiuchumi wa Iran na ameshafanya mazungumzo na waziri mwenzake wa mambo ya nje wa Mali, Abdoulaye Diop.

Mbali na kuonana na viongozi wa ngazi za juu wa Mali, lengo jingine la ziara ya Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran nchini humo ni kushuhudia vikifanyika vikao vya kamisheni za pamoja za kiuchumi za nchi mbili.

Abdollahian aliwasili Bamako, mji mkuu wa Mali jana usiku na kupokewa na mwenyeji wake, Abdoulaye Diop.

Mara baada ya kuwasili nchini humo, Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran amesema, ziara yake hiyo yenye ujumbe wa ngazi za juu wa kisiasa na kiuchumi, onaonesha nia ya kweli ya Jamhuri ya Kiislamu ya kuimarisha uhusiano na ushirikiano wake na nchi za Afrika ikiwemo Mali katika nyuga muhimu hasa za kisiasa na kiuchumi.

Amesema tena, na kwa kusisitiza kwamba, kuimarisha uhusiano wa kiuchumi na kisiasa na Mali na kupandisha kiwango cha mabadilishano ya bidhaa na kibiashara baina ya pande mbili, ni katika mipango maalumu ya serikali ya hivi sasa ya Iran.

Inafaa kukumbusha hapa kuwa, miongoni mwa wajumbe waliomo kwenye ujumbe huo wa ngazi za juu wa Iran unaoongozwa na Waziri wa Mambo ya Nje, Hossein Amir-Abdollahian, ni wawakilishi wa sekta binafsi na za kiserikali wa Jamhuri ya Kiislamu.

 

Previous Post
Next Post

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *