Wanajeshi wa Israel waendeleza jinai katika maeneo tofauti ya Palestina

Wanajeshi wa utawala wa Kizayuni wanaendelea na jinai zao dhidi ya Wapaelstina katika eneo la Ukingo wa Magharibi wa Mto Jordan.

Kanali ya Telegram ya al Risala imesambaza mkanda wa video leo Jumanne unaoonesha jinai za wanajeshi makatili wa Israel na jinsi wanavyovamia na kufanya ukatili dhidi ya Wapalestina katika mji wa al Khalil wa Ukingozo wa Magharibi wa Mto Jordan.

Katika upande mwingine, kanali ya habari ya al Quds nayo imesambaza video kwenye mtandao wa kijamii wa Telegram na kuandika, wanajeshi vamizi wa Israel wamevamia kitongoji cha Silwad kaskazini mwa Ramallah na kufanya mashambulio dhidi ya raia wa Palestina.

Wapalestina wa kitongoji hicho nao wamejibu mashambulizi hayo ya wanajeshi makatili wa Israel ingawa kwa silaha zao hizo hizo nyepesi za mawe n.k.

Jana Jumatatu, Mahmoud al Zahar, mmoja wa viongozi wa ngazi za juu wa Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Palestina HAMAS aligusia mapambano ya harakati za Palestina katika Ukingo wa Magharibi na kusema: “Harakati za muqawama na mapambano katika Ukingo wa Magharibi zimepelekea utawala wa Kizayuni wa Israel uingiwe na kiwewe na uchanganyikiwe kwani hali katika eneo hilo ni sawa na ya mapambano ya Ukanda wa Gaza.”

Alisema, hivi sasa kunashuhudiwa mauaji ya Wapalestina yakifanywa na Wazayuni kila leo katika Ukingo wa Magharibi na hilo linaashiria kushika kasi mapambano ya kishujaa na muqawama wa kupigiwa mfano wa Wapalestina wa eneo hilo.

Previous Post
Next Post

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *