Waziri wa Mashauri ya Kigeni wa Iran akutana na Rais wa Zanzibar

Waziri wa Mashauri ya Kigeni wa Jamhuri ya Kiislamu7 ya Iran aliyeko ziarani nchini Tanzania leo amekutana na kufanya mazungumzo na Rais Hussein Mwinyi wa Zanzibar na wawili hao wamesitizia udharura wa kuimarishwa ushirikiano baina ya pande mbili.

Rais Hussein Mwinyi wa Zanzibar ameashiria katika mazungumzo yake na Hussein Amir-Abdollahian kuhusu uhusiano mkongwe baina ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran na Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na kusisitiza kwamba, ana matumaini kuwa, uhusiano huo utaimarishwa zaidi na kupelekea kukuzwa ushirikiano wa Iran na visiwa vya Zanzibar.

Rais Mwinyi amesema kuwa: Tunaishukuru Iran kutokana na himaya na uungaji mkono wake kwa Zanzibar na nitafurahi kushiriki katika vikao vya pande mbili.

Kabla ya hapo, Amir-Abdollahian alikutana na kufanya mazungumzo na Nassor Ahmed Mazrui, Waziri wa Afya wa Zanzibar .

Katika mazungumzo yake na Hussein Amir-Abdollahian, Waziri wa Afya, Ustawi wa Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto wa Zanzibar alisema anatumai kuwa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran na Jamhuri ya Muungano wa Tanzania zitaimarisha na kupanua uhusiano wao wa pande mbili.

Amir-Abdollahian aliwasili katika uwanja wa ndege wa Zanzibar Jumatano jioni, na kukaribishwa na Nassor Ahmed Mazrui, Waziri wa Afya wa Zanzibar na viongozi wengine wa visiwa hivyo.

Aidha akiwa jijini Dar es Salaam hapo jana, Waziri wa Mashauri ya Kigeni wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran aliyeko ziarani nchini Tanzania katika ziara ya kulitembelea bara Afrika akitokea Mali alisema kuwa, Afrika ni moja ya vipaumbele vikuu vya diplomasia ya kiuchumi ya Iran.

 

Previous Post
Next Post

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *