Mikhail Gorbachev, kiongozi wa mwisho wa Muungano wa Jamhuri za Kisoshalisti za Sovieti (Union of Soviet Socialist Republics, USSR) alifariki dunia Jumanne usiku katika hospitali moja mjini Moscow, Russia akiwa na umri wa miaka 91 baada ya kuugua kwa muda mrefu.
Japokuwa barua ya kihistoria ya Imam Khomeini kwa Gorbachev ilitolewa katika hali ya kushtukiza na isiyotarajiwa, ukizingatiwa pia uchambuzi wa kina aliofanya Imam Khomeini katika barua hiyo, lakini inaonesha kuwa, chimbuko lake linarejea katika historia ya Iran na Muungano wa Sovieti. Kwa upande mmoja, barua hiyo ilikuwa hatua muhimu na ya msingi zaidi kuchukuliwa na Imam Khomeini katika suala la kuyatangaza na kuyafikisha Mapinduzi nje ya nchi; na kwa upande mwingine, lilikuwa onyo muhimu zaidi lililotolewa kuhusiana na mchakato wa mageuzi yaliyokuwa yakifanywa na Muungano wa Sovieti katika zama hizo.