Operesheni za kupambana na jinai za Wazayuni zimeongezeka sana 2022

Operesheni za kupambana na jinai za utawala wa Kizayuni wa Israel katika Ukingo wa Magharibi wa Mto Jordan zimeongezeka sana mwaka huu wa 2022.

Hayo yametangazwa na shirika la habari la Shahab ambalo limeongeza kuwa, zaidi ya opereseheni 7,200 za muqawama wa wananchi wa Palestina zimeshafanyika katika Ukingozo wa Magharibi wa Mto Jordan tangu mwanzoni mwa mwaka huu 2022 hadi hivi sasa.

Kila siku walowezi wa Kizayuni wanatumia visingizio mbalimbali kufanya jinai dhidi ya wananchi wasio na ulinzi wa Palestina lakini hivi sasa Wapalestina nao wameamua kutokaa tena kimya, bali wameanzisha operesheni za mtawalia za kujihami mbele ya vitendo na jinai hizo za utawala wa Kizayuni.

Kwa mujibu wa ripoti ya shirika la habari la Shahab, mwezi Januari mwaka huu, kulifanyika operesheni 623 za wanamapambano wa Palestina dhidi ya utawala wa Kizayuni katika Ukingo wa Magharibi wa Mto Jordan ambapo matukio 28 kati yake yalikuwa ni ya kupigwa risasi Wazayuni. Mwezi uliofuata wa Februari 2022 opereshenei hizo ziliongezeka na kufikia 835 ambapo 52 kati yake zilikuwa ni operesheni za kupigwa risasi Wazayuni makatili.

Mwezi Machi pia, operesheni hizo za muqawama wa Palestina zilifikia 821 na mwezi Aprili pia idadi ya operesheni hizo iliongezeka mno na kufikia 1,510 huku matukio 76 kati yake yakiwa ni ya operesheni za kupigwa risasi Wazayuni katika Ukingo wa Magharibi wa Mto Jordan.

Katika kipindi cha masaa 24 yaliyopita pia, kumeripoti operesheni 14 za kushambuliwa walowezi wa Kizayuni katika maeneo tofauti ya Ukingo wa Magharibi wa Mto Jordan.

Previous Post
Next Post

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *