Kamanda wa Jeshi la Anga la Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesema kuwa Iran inajitosheleza katika uundaji wa ndege zisizo na rubani (droni).
Sekta ya ulinzi ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran baada ya ushindi wa Mapinduzi ya Kiislamu hadi leo imekuwa na mafanikio mbalimbali nchini katika nyanja mbalimbali za nchi kavu, baharini, anga, na makombora. Aidha hivi sasa Iran ina uwezo wa kujilinda dhidi ya tishio lolote dhidi la kimataifa dhidi yake kwa kupiga hatua kubwa uwezo wa kiulinzi wa nchi hii; ambapo hii leo Jamhuri ya Kiislamu ya Iran inajulikana kama nguvu ya kieneo.
Katika uwanja huo, Brigedia Jenerali Hamid Vahedi Kamanda wa Jeshi la Anga la Jamhuri ya Kiislamu ya Iran akiwa pambizoni mwa kukagua uwezo wa kivita wa kambi ya Anga ya Shahid Fakuri huko Tabriz katika mkoa wa Azerbaijan Mashariki amesema: ” tumekuwa na mafanikio mazuri katika sekta ya ndege zisizo na rubani, ambapo jeshi la anga limeunda droni mbili za kimkakati sana na za thamani kubwa kwa majina ya Kaman 12 na Kaman 22 na Wizara ya Ulinzi ya Iran imeunda ndege nyingine zisizo na rubani.
Kamanda wa Jeshi la Anga la Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesema: tunazitangazia wazi nchi zote jirani kwamba, doktrini yetu ya kijeshi ni ya kwa ajili ya kujilinda na wala hatuna jicho la tamaa kwa nchi yoyote.”