Jumuiya ya Mashabiki wa Soka Uingereza (FSA) imetoa mwito wa mashabiki kurejeshewa pesa walizotoa kwa ajili ya kununua tiketi za kushuhudia michuano ya mpira wa miguu; lakini baadaye ikaakhirishwa kufuatia kifo cha Malkia Elizabeth II wa nchi hiyo.
Mwenyekiti wa jumuiya hiyo, Malcolm Clarke ameyataka mashirika na mamlaka zinazosimamia kandanda nchini humo kuhakikisha kuwa mashabiki waliokuwa wamenunua tiketi za kushuhudia meci mbalimbali nchini humo wanarejeshea fedha zote.
Clarke amesema: Kuna suala zito la kurejeshewa fedha na tiketi za treni walizokata mashabiki mapema kabla ya michuano iliyotazamiwa kupigwa nje ya miji yao.
Usimamizi wa soka nchini humo umetangaza kuakhirisa mechi zote, kuanzia zile za daraja za chini hadi za Ligi Kuu ya Soka ya Uingereza (EPL), kwa heshima ya kufariki dunia Malkia Elizabeth.
Ifahamike kuwa, Malkia Elizabeth alikuwa mlezi wa Shirikisho la Soka Uingereza (FA), ambali limetangaza kuakhirishwa kwa mechi zote za mpira wa miguu kipindi hiki cha kuomboleza kifo cha mtawala huyo wa kifalme aliyoingoza Uingereza kwa miaka 70.
Hivi karibuni pia, ripota na mwanasoka wa zamani wa Uingereza amepinga ubaguzi wa rangi katika jamii ya nchi hiyo wakati wa utawala wa Malkia Elizabeth II aliyeaga dunia Alkhamisi iliyopita akiwa na umri wa miaka 96. Trevor Sinclair ambaye sasa ni kocha na mtaalamu wa soka, aliandika ujumbe kwenye mtandao wa Twitter unaosema: “Ubaguzi wa rangi umekithiri nchini Uingereza, hivyo watu weusi na Waasia hawapaswi kuomboleza kifo cha Malkia Elizabeth.”