Israel yafanya maneva ya kijeshi katika Ghuba ya Haifa kwa kuhofia maonyo ya Hizbullah

Utawala wa Kizayuni wa Israel umetangaza kuwa unafanya maneva ya kijeshi kuanzia Ghuba ya Haifa hadi katika mpaka wa baina ya Palestina inayokaliwa kwa mabavu na Lebanon kwa kuhofia indahri za karibuni za harakati ya Hizbullah ya Lebanon.

Msemaji wa jeshi la Israel ameeleza kuwa, mazoezi hayo ya kijeshi yameanza mapema leo katika mpaka wa Lebanon na yatamalizika leo jioni.

Mapema Septemba 4 mwaka huu jeshi la Kizayuni lilitangaza kuanza kwa maneva ya kijeshi ya siku tatu karibu na mpaka wa Lebanon.

Maneva haya ya kijeshi yanafanyika huku mvutano ukiongezeka kati ya harakati ya Hizbullah na utawala wa Tel Aviv kuhusu hatua ya utawala huo ya kutaka kuchimba mafuta na gesi katika eneo la Karish linalopatikana katika maji ya Lebanon.

Tarehe 29 Agosti harakati ya Hizbullah ya Lebanon ilitahadharisha kuwa inafuatilia kikamilifu meli za utawala wa Kizayuni zilizoelekea katika mpaka wa Lebanon na Palestina inayokaliwa kwa mabavu kwa lengo la kuchimba mafuta na gesi.

Israel ilipanga kuchimba gesi katika medani ya Karish, hata hivyo imeakhrisha zoezi hilo kwa kuhofia indhari za Hizbullah. Sayyid Hassan Nasrullah, Katibu Mkuu wa Hizbullah alisema mwezi Juni mwaka huu kwamba adui asiruhusiwe kuchimba gesi katika medani ya Karish na akasisitiza kuwa utawala wa Kizayuni hauwezi kulilinda mtambo unaloelea majini na kuendeleza mchakato wa uchimbaji wa gesi.

 

Previous Post
Next Post

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *