Aghalabu ya Wademocrat wanatilia shaka iwapo Biden atagombea urais 2024

Akthari ya wafuasi na wanachama wa chama cha Democrat nchini Marekani wametilia shaka uwezekano wa Rais Joe Biden wa nchi hiyo wa kugombea muhula wa pili katika uchaguzi ujao wa rais wa mwaka 2024.

Utafiti wa hivi karibuni uliofanywa na USA Today ikishirikiana na Ipsos unaonesha kuwa, asilimia 56 ya wapigakura wa chama cha Democratic hawaungi mkono azma ya Biden ya kuwania urais katika uchaguzi mkuu ujao wa 2024.

Asilimia 59 ya wafuasi wa chama hicho tawala wanahisi kuwa, mtangulizi wa Biden, Donald Trump ‘anastahili’ kuchaguliwa tena katika uchaguzi ujao.

Kwa mujibu wa utafiti huo wa maoni, asilimia 82 ya wafuasi wa Republican wanaamini kuwa Trump ana nafasio kubwa ya kushinda uchaguzi wa rais 2024.

Utafiti mwingine uliofanywa na jumuiya ya Convention of States unaonesha kuwa, asilimia 58.7 ya wapigakura walioshiriki kwenye utafiti huo wanaitakidi kuwa, Biden ameligawa taifa hilo, huku asilimia 20.6 pekee wakiamini kuwa amewaunganisha na kuwaleta pamoja wananchi wa nchi hiyo.

Haya yanajiri siku chache baada ya utafiti mwingine uliotolewa Jumatatu iliyopita na shirika la Trafalgar kuonesha kuwa, Biden amevunja rekodi ya kushuka umashuhuri wake baina ya Wamarekani. Utafiti huo unasema kuwa, umaarufu wa Biden umeshuka hadi kiwango cha chini kabisa na kufikia asilimia 39.

Previous Post
Next Post

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *