Mbunge wa Bunge la Ulaya: Marekani na Israel zinaunga mkono ugaidi

Mick Wallace, Mwakilishi wa Ireland katika Bunge la Ulaya amekosoa vikali sera za Marekani na utawala ghasibu wa Israel na kuzitaja kuwa waungaji mkono wa ugaidi.

Mbunge huyo wa Bunge la Ulaya amelaani mauaji ya kizazi ya Saudi Arabia na Imarati huko nchini Yemen na kutangaza kuwa, Marekani na utawala wa Kizayuni wa Israel zinaunga mkono ugaidi.

Kadhalika Mick Wallace amekosoa vikali pia msimamo wa Bunge la Umoja wa Ulaya kuhusiana na shauku na sera za Marekani, mataifa ya Ulaya, Israel, Saudi Arabia na Imarati za kupenda vita.

Mwakilishi huyo wa Ireland katika Bunge la Ulaya kadhalika amesema, wakati Ufaransa, Uingereza na mataifa mengine yanapozipatia silaha Saudi Arabia na Imarati ili zifanye mauaji ya kizazi nchini Yemen je huu siyo ugaidi?

Aidha amewalaumu wawakilishi katika Bunge hilo la Umoja wa Ulaya na kuwahoji kwamba, wanataka kuamka lini na kuachana na kimya chao cha kufumbia macho ukweli na kuanza maisha mapya katika ulimwengu huu?

Kuuza silaha ni mojawapo ya sera kuu za kiuchumi na kisiasa za nchi za Magharibi, ambazo kupitia mauzo ya silaha hizo hupata mabilioni ya dola kila mwaka. Silaha hizo zinauziwa zaidi nchi ambazo zimo katika orodha ya wavunjaji wa haki za binadamu, hivyo katika miaka ya hivi karibuni na kwa kuendelea vita vya kidhalimu vya Saudia dhidi ya Yemen, Riyadh imekuwa miongoni mwa wanunuzi wakubwa wa silaha kutoka nchi za Ulaya.

Previous Post
Next Post

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *