Mlipuko wa bomu lililotegwa kwenye gari na shambulio la silaha katika hoteli moja nchini Somalia

Vyanzo vya habari nchini Somalia vimeripoti mlipuko wa bomu lililotegwa ndani ya gari mbele ya hoteli moja katika mji wa pwani wa Kismayo na shambulio la kutumia silaha.

Jumapili hii mwendo wa saa sita mchana, watu wenye silaha walilenga Hoteli iitwayo ‘Tawakkel’ katikati mwa Kismayo, mji mkuu wa jimbo la Jubaland, kwa bomu lililotegwa ndani ya gari.

Taarifa za awali zinaonyesha kuwa watu wa kundi la kigaidi la Al-Shabaab walishambulia hoteli hiyo baada ya kulipua bomu lililokuwa limetegwa ndani ya gari mbele ya hoteli hiyo.

Kulingana na ripoti ya tovuti ya Al-Somal Al-Jadeed, hivi sasa kuna mzozo kati ya washambuliaji na vikosi vya usalama na walinzi wa hoteli.

Kundi la kigaidi la Al-Shabaab lenye mafungamano na Al-Qaeda limedai kuhusika na shambulio hili

Previous Post
Next Post

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *