Syria: Tunataka uanzishwe mfumo mpya wa kimataifa, jinai za Israel zidhibitiwe

Kwa mnasaba wa Siku ya Umoja wa Mataifa, Serikali ya Syria imetoa wito na kusisitiza ulazima wa kuundwa mfumo mpya wa kimataifa na kuzuiwa uchokozi wa utawala wa Kizayuni wa Israel na jinai zinazofanywa na utawala huo haramu.

Kwa mujibu wa kituo cha televisheni cha Al-Akhbariya; Wizara ya Mambo ya Nje ya Syria imetoa taarifa kwa mnasaba wa Siku ya Umoja wa Mataifa na kutangaza kuwa: kutoheshimiwa na nchi za Magharibi Hati ya Umoja wa Mataifa na kutekelezwa sera za uvamizi, ukoloni, utumiaji vigezo vya kiundumakuwili na kupora utajiri wa nchi zinazoendelea vimeuweka mbali Umoja wa Mataifa na jukumu lake na kuuondoa kwenye nafasi yaka inayotakiwa.
Taarifa hiyo imefafanua kuwa: kama ilivyokuwa huko nyuma, Syria inataka uanzishwe mfumo mpya wa kimataifa unaoheshimu Hati ya Umoja wa Mataifa, kuhitimishwa sera za kibabe na ubeberu wa kikoloni, na kuzuia hatua za utawala ghasibu wa Israel na jinai zake katika maeneo ya nchi za Kiarabu unayoyakalia kwa mabavu, na kuandaa mazingira ya kujenga ulimwengu mpya ambao ndani yake mataifa yataweza kupata haki zao, demokrasia kutawala uhusiano wa kimataifa, na ulimwengu mzima kunufaika na ustawi endelevu.

Katika miaka ya hivi karibuni, utawala wa Kizayuni wa Israel umekuwa ukifanya mashambulio ya mara kwa mara ya anga dhidi ya mji mkuu wa Syria Damascus na maeneo mengine tofauti ya nchi hiyo ingwa mara nyingi hujuma na mashambulio hayo yamekuwa yakizimwa na mitambo ya ulinzi wa anga ya nchi hiyo.

Uvamizi na mashambulizi ya anga ya utawala wa Kizayuni yanaendelea kufanywa wakati serikali ya Syria imeshatuma barua mara kadhaa kwa Umoja wa Mataifa kulaani mashambulizi hayo na kutaka yakomeshwe.
Previous Post
Next Post

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *