Russia: Marekani na Ulaya zinataka kuwafanya walimwengu waghafilike na kadhia ya Palestina

Balozi na mwakilishi wa kudumu wa Russia katika Umoja wa Mataifa amesema kuwa, Marekani na Ulaya ndio wahusika wakuu wa kushadidi mgogoro wa Palestina.

Vasily Nebenzya, Balozi na mwakilishi wa kudumu wa Russia katika Umoja wa Mataifa amesisitiza kuwa, umewadia wakati sasa kwa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa kuchuukua hatua za kurekebisha hali hii.

Mwanadiplomasia huyo wa Rusia amebainiisha kuwa, Marekani na Ulaya zinataka kuwapotosha walimwengu na hivyo kuwafanya wasiuzingatie na kuupa umuhimu mgogoro wa Palestina na utawala wa muda wa Israel.

Ameongeza kuwa, kwa hakika Baraza la Usalama linadaiwa na Wapalestina. Ni kwa makumi ya miaka sasa ambapo maazimio ya Baraza la Usalama na Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa hayatekelezwi.

Balozi na mwakilishi wa kudumu wa Russia katika Umoja wa Mataifa amesisitiza kuwa, misimamo ya kindumakuwili ya Marekani na madola ya Ulaya pamoja na uungaji mkono wao kwa utawala ghasibu wa Israel ni mambo ambayo kwa hakika yanayafanya mataifa hayo kuwa na hisa kubwa ya halii mbaya inayowakumba Wapalestina hii leo.

Asasi za kimataifa kama Umoja wa Mataifa na baraza lake la usalama zinakosolewa na kulaumiwa vikali kutokana na kutochukua hatua za maana za kukabiliana na hatua mbalimbali zisizo za kibinadamu zinazofanywa na utawala ghasibu wa Israel huko Palestina sambamba na uvamizi wa mara kwa mara wa walowezi wa Kiyahudi dhidi ya msikiti mtakatifu wa al-Aqswa.

Previous Post
Next Post

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *