Kampuni ya Uingereza yagundulika kuhusika na kashfa ya kueneza saratani Iraq

Tovuti moja ya habari mefichua kuwa kampuni ya Uingereza inayofanya kazi katika maeneo ya mafuta ya Iraq ni moja ya sababu kuu za kuenea kwa saratani nchini humo.

Tovuti moja ya habari imefichua kwamba Kampuni ya Petroli ya Uingereza ilisababisha kuenea kwa uugonjwa wa saratani nchini Iraq, lakini vyombo vya habari vya Magharibi na hasa vya Uingereza vinajaribu kuficha suala hili na kutoruhusu kuchapishwa kwa habari za uhusiano wa kampuni hiyo na kuenea kwa ugonjwa wa kansa nchini Iraq.

Ripoti ya vyombo vya habari vya Iraq inasema, jamii ambazo zinaishi karibu na maeneo ya mafuta na ambapo gesi inayotolewa kutoka kwenye visima huchomwa kwenye hewa ya wazi, ziko katika hatari kubwa ya kupata saratani ya damu.

Ripoti hiyo imesema, inaelezwa kuwa kuchomwa kwa gesi na mafuta kumesababisha kuenea kwa uchafuzi wa kansa katika maeneo jirani, na kwamba eneo baya zaidi limerekodiwa katika viunga vya mkoa wa Basra kusini mwa Iraq, ambao una kiwango cha juu zaidi cha uchafuzi wa mazingira.

Vyombo vya habari vya Iiraq vimesisitiza kwamba kwa kutumia takwimu zilizopatikana kutoka kwa satelaiti, inawezekana kuthibitishwa kuwa medani ya mafuta wa Al-Ramila, aeneo kubwa la mafuta huko Basra ambalo mkandarasi wake ni British Petroleum, huchoma gesi nyingi kutoka kwenye visima kuliko medani nyingine yoyote ya gesi duniani.

Umoja wa Mataifa umetangaza kwamba maeneo hayo ya kusini mwa Iraq, ndiyo yaliyoathiriwa hivi karibuni katika orodha ya kesi za haki za binadamu.

Previous Post
Next Post

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *