Raia mmoja wa Marekani mwenye asili ya Afrika ameachiwa huru baada ya kufungwa jela kwa karibu miongo minne kwa kosa ambalo hakulifanya.
Maurice Hastings, 69, aliachiwa huru jana Ijumaa katika jimbo la California , baada ya vipimo vya msimbojeni (DNA) kuonesha kuwa hakuhusika na kosa la mauaji aliyodaiwa kufanya.
Ofisi ya Mwanasheria wa Wilaya ya Kaunti ya Los Angeles imemuachia huru Hastings, na kukiri kuwa alihukumiwa na kufungwa kimakosa, kwa madai ya kumteka nyara na kumuua Roberta Wydermyer, 30, katika jiji la Inglewood mwaka 1983.
Vipimo vipya vya vinasaba (DNA) vimemuondoa hatiani raia huyo mweusi wa Marekani, na kutambua mtu mwingine kuwa mhusika wa mauaji hayo.
Ofisi ya Mwanasheria wa Wilaya ya Kaunti ya Los Angeles hata hivyo imesema mhusika halisi wa mauaji hayo ya mwaka 1983 alifia gerezani mwaka 2020, akitumikia kifungo cha mashitaka tofauti ya utekaji nyara na ubakaji.
Mwanasheria katika Wilaya ya Kaunti ya Los Angeles, George Gascon sanjari na kumuomba radhi Hastings kwa kufungwa miaka 38 ‘kimakosa’ amekiri kuwepo mapungufu katika mfumo wa mahakama wa Marekani.
Afisa huyo wa serikali amesema akimhutubu Hastings kwamba, “Mfumo ulikufeli, mfumo ufeli wahanga wengi, upo huru leo kutokana na uvumilivu wako.”
Matokeo ya uchunguzi huo uliofanywa na taasisi ya Gallup yanaonesha kuwa, asilimia 64 ya Wamarekani waamini kuwa, ubaguzi wa rangi dhidi ya watu weusi umekithiri nchini Marekani na kwamba kiwango hicho ni kikubwa zaidi tangu mwaka 2008.
Mauaji yaliyofanywa na afisa mmoja Mzungu wa polisi ya Marekani dhidi ya Mmarekani mweusi George Floyd tarehe 25 Mei mwaka 2020, ulionesha kukiti mizizi ya ubaguzi nchini humo. Ukatili huo ulizusha maandamano ndani na nje ya Marekani.