Azimio la mwisho la maandamano ya Siku ya Taifa ya Kupambana Ubeberu

Washiriki katika maandamano ya Siku ya Taifa ya Kupambana na Ubeberu inayosadifiana na leo 4 Novemba, wamesisitiza udharura kuwepo mapambano endelevu dhidi ya njama za kuzusha fitna, ghasia na fujo.

Washiriki katika maandamano ya leo ya kupinga ubeberu wa kimataifa ambao walikuwa wakipiga nara za “Mauti kwa Marekani” kuonyesha kuchukizwa kwao na siasa za kiuadui na kibeberu za mfumo wa ubeberu unaoongozwa na serikali ya Washington, wametangaza uungaji mkono wao kwa hatua za kimapinduzi za Bunge, Serikali na Idara ya Mahakama hapa nchini na kusisitiza udharura wa kudumishwa mapambano dhidi ya wanaozusha fitina na ghasia. Vilevile azimio lililotolewa mwishoni mwa maandamano hayo limewataka viongozi wa nchi kutofautisha baina ya watu walioeleza malalamiko yao katika matukio ya hivi karibuni hapa nchini na wale wanaozusha ghasia na fujo, na kutayarisha mazingira ya kisheria ya ukosoaji wa wananchi.

Azimio la mwisho la maandamano ya leo pia limewaenzi mashahidi waliouawa katika shambulio la kigaidi katika Haram Tukufu ya Hadhrat Ahmad Ibn Musa (AS) huko Shiraz na kusema: Jinai hiyo ya kutisha na kimya cha wanaodai kutetea haki za binadamu ni ushahidi wa kina cha chuki na kielelezo cha uovu wa dhalimu mkubwa, Marekani, na ni alama ya mkono wa adui muwasha moto na vibaka wake wasaliti, majahili na walioghafilika dhidi ya taifa kubwa la Iran ya Kiislamu.

Katika azimio hilo imeelezwa kuwa: Washiriki wa maandamano 13 Aban (4 Novemba) wakiwa na uelewa mzuri kuhusu ubeberu wa kimataifa, wanafahamu vyema kwamba njama za mashirika ya ujasusi ya Marekani, Uingereza na utawala wa Kizayuni na unaoua watoto wa Israel, na kwa msaada wa tawala fasidi za Al-Saud na Uingereza, na hujuma za mtandaoni zisizo na kifani na kwa usaidizi wa watu mashuhuri vibaraka waliopoteza utambulisho wao ambao wamefeli katika ghasia za hivi karibuni, hawataacha kuwaandama vijana wa nchi hii; kwa msingi huo familia, walezi, walimu na wahadhiri walioelimika na maafisa wa masuala ya utamaduni wa nchi wanaombwa kulipa uzito suala la kubainisha ukweli na kuzima njama na mipango ya maadui kwa kudumisha umakini, kuwasiliana na kufanya mazungumza na kizazi kipya.

Washiriki katika maandamano ya Siku ya Taifa ya Kupambana na Ubeberu wa Kimataifa pia wamewashukuru wanafunzi na walimu walioko mstari wa mbele katika hatua ya pili ya Mapinduzi ya Kiislamu, ambao wamesimama imara dhidi ya makundi yanayofanya uchochezi katika vituo vya elimu.

Previous Post
Next Post

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *