Vyombo vya habari vya Israel: Miaka 25 ijayo, utawala wa Kizayuni utakuwa umeshatoweka

Matokeo ya uchunguzi wa maoni uliofanywa Israel yanaonyesha kuwa theluthi moja ya walowezi wa Kizayuni hawataki kuajiriwa jeshini na wanaamini kuwa nchi iitwayo Israel haitakuwepo tena baada ya miaka 25.

Kwa mujibu wa televisheni ya Al-Mayadeen, baadhi ya vyombo vya habari vya Israel vimefichua kuwa thuluthi moja ya vijana wa Israel hawaamini kama Israel itakuwepo baada ya miaka 25.

Kwa mujibu wa matokeo ya uchunguzi uliofanywa na muungano wa mavuguvugu ya vijana wa Kizayuni na kutangazwa na kanali ya 12 ya televisheni ya utawala wa Kizayuni, thuluthi moja ya vijana wa Israel hawataki kuajiriwa jeshini.

Chaneli hiyo ya televisheni ya Israel imeendelea kubainisha kuwa, taarifa hizo ni “hatari na za kusononesha moyo”.

Previous Post
Next Post

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *