Biden apatwa na wahka: Nitauzuliwa iwapo Warepublican watashinda uchaguzi

Rais wa Marekani amekiri kwamba atakabiliwa na hatari ya kuitwa bungeni kwa ajili ya kusailiwa na kutimuliwa iwapo Warepublican watachukua udhibiti wa Bunge la Congress katika uchaguzi wa katikati ya muhula.

Rais wa Marekani, Joe Biden, amekiri kwamba iwapo Warepublican watashinda uchaguzi huo na kulidhibiti Bunge la Congress Jumanne ya kesho, yumkini akasailiwa na kutimuliwa.

Biden ametoa matamshi hayo alipokuwa akimpigia debe mwakilishi wa chama cha Democratic, Mike Levin, ambaye anawania tena kiti cha eneo bunge la 49 huko California.

Baadhi ya Warepublican katika Congress wameelezea hamu yao ya kuibua vifungu vya kumsaili na kumtimua Joe Biden iwapo chama cha Republican kitachukua udhibiti wa Baraza la Wawakilishi na hata Seneti katika uchaguzi wa katikati ya muhula.

Matokeo ya uchunguzi wa Gallup yalionyesha kuwa viashiria vyote vya kitaifa vinavyohusiana na hali ya umma katika mkesha wa uchaguzi wa katikati ya muhula wa Novemba 8 wa Bunge la Merekani vinaonesha kuwa chama cha Republican kitaibuka na ushindi.

Utendaji mbaya wa serikali ya Biden kama rais wa Merekani umeweka hatarini hatima ya chama cha Democratic katika uchaguzi wa Bunge la Congress.

Previous Post
Next Post

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *