Kundi la kwanza la wanajeshi wa Kenya latua mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo

Wanajeshi wa Kenya jana Jumamosi walitua katika mji wa Goma mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo’ ambapo walilakiwa na maafisa husika na wanajeshi wa Kongo katika eneo.

Wanajeshi wa Kenya wamewasili katika mji wa Goma wakati kundi la waasi la M23 likiwa limeingia katika jimbo la Kivu Kaskazini la Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, na kuteka maeneo mengi na hivyo kuzidisha  hali ya wasiwasi katika eneo la Maziwa Makuu.

Guillaume Ndjile Msemaji wa jeshi la Kongo huko Kivu ya Kaskazini ameeleza kuwa maagizo yaliyotolewa na wakuu wa nchi, lakini pia lengo liko wazi kabisa. Marafiki wetu kutoka Kenya wako hapa kwa ajili ya kutekeleza oparesheni za kukabiliana na makundi yenye silaha. Wanajeshi wa Kenya wameelekea mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo baada ya bunge la Kenya kupasisha kutumwa huko Kongo wanajeshi wa nchi hiyo zaidi ya 900.

Itakumbukwa kuwa mwezi Juni mwaka huu viongozi wa Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) walipendekeza kuundwa kikosi cha pamoja cha kijeshi. kamanda wa kikosi cha Kenya kilichowasili mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo Luteni kanali Obiero Denis amebainisha wazi malengo yao na kusema:tuna majukumu ya kutima ambayo yamegawanyika katiak sehemu nne. Jukumu la kwanza ni kushirikiana pamoja na wenzetu katika jeshi la Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo ili kutokomeza makundi  hasi ya wanamgambo, na pili ni kufanya kazi na jumuiya ya misaada ya kibinadamu ili kuwasaidia wakimbizi wa ndani.”

Shirika la Umoja wa Mataifa la  misaada ya kibinadamu linakadiria kuwa mapigano ya hivi majuzi huko Kivu Kaskazini yamesababisha zaidi ya watu 180,000 kuzihama nyumba zao.

Previous Post
Next Post

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *