Wazayuni waingiwa na hofu baada ya Netanyahu kupewa jukumu la kuunda serikali mpya Israel

Sambamba na Benjamin Netanyahu kupewa jukumu la kuunda baraza la mawaziri la serikali mpya ya Israel, mmoja wa majenerali wa Israel ameutaja uteuzi wake kuwa ni maafa makubwa.

Jenerali Amos Gilad wa Israel na mkuu wa zamani wa Idara ya Usalama na Siasa ya Wizara ya Vita ya utawala huo ameutaja uteuzi wa mawaziri wa serikali ijayo ya Israel kuwa ni “janga kubwa”.

Jenerali huyo wa Kizayuni ametahadharisha kuhusu maafa makubwa yatakayotokea iwapo Benjamin Netanyahu atamteuwa Bezalel Yoel Smotrich, mkuu wa Chama cha Kidini cha Uzayuni, kuwa Waziri wa Vita katika baraza la mawaziri la baadaye la utawala huo.

Jenerali Amos Gilad amesema, ni maafa makubwa iwapo Netanyahu atamteuwa Bezalel Smotrich kuwa waziri wa vita wa Israel.

Itakumbukwa kuwa, Rais Yitzhak Herzog wa Israel amemteua rasmi Benjamin Netanyahu, kiongozi wa chama cha Likud kuunda baraza la mawaziri baada ya kushinda uchaguzi wa Knesset (Bunge la utawala wa Kizayuni).

Sasa Netanyahu ana siku 28 kuunda baraza lake la mawaziri;  na iwapo atashindwa kuunda serikali mpya ndani ya siku 14 baada ya kumalizika muhula huo wa siku 28, itabidi uchaguzi wa Knesset ufanyike tena.

Hofu kuhusu baraza la mawaziri la serikali ijayo ya utawala wa Kizayuni chini ya Uongozi wa Benjamin Netanyahu na Wazayuni wenzake wenye misimamo ya kupindukia mipaka, imetanda katika duru mbalimbali za kikanda na kimataifa.

 

Previous Post
Next Post

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *