Vyombo vya habari vya Kizayuni vimetuma timu kadhaa za waandishi na wataalamu wa vyombo vya habari kwenye Kombe la Dunia nchini Qatar; Miongoni mwa waandishi hao ni “Ohad Ben Hamo,” mwandishi wa habari wa Israel ambaye anajulikana kuwa ni mtaalamu wa masuala ya Waarabu na Wapalestina.
Ben Hamo, ambaye anaelewa vizuri lugha ya Kiarabu, ni Mzayuni mwenye chuki ambaye anajigamba waziwazi kuwa yeye ni Mzayuni.
Siku chache zilizopita, amejaribu sana kufanya uchunguzi wa maoni kupitia kuwahoji mashabiki wa nchi za Kiarabu katika mashindano ya Kombe la Dunia yanayoendelea nchini Qatar hivi sasa kuhusiana na kiwango cha kukubalika utawala wa Kizayuni katika ulimwengu wa Kiarabu. Lakini jambo la kushangaza lililomkirihisha vibaya Mzayuni huyo ni kwamba hakuna hata raia mmoja wa Qatar, wala Saudia, wala Morocco, wala Bahrain na wala Muungano wa Falme za Kiarabu yaani Imarati aliyekuwa tayari kuzungumza naye. Kila alipokuwa anajitambulisha kuwa yeye ni ripota kutoka Israel, watu wote walimkwepa kama ukoma na kama mtu mwenye ugonjwa hatari wa kuambukiza.
Kama aibu hiyo aliyopata haikutosha, vijana wa Lebanon, Palestina na Tunisia na vijana wengine kutoka nchi za Ghuba ya Uajemi zwalimzunguka wakishikilia bendera ya Palestina na kusema kwa sauti kubwa, hakuna nchi iitwayo Israel.
Baada ya kukumbwa na fedheha hiyo, Mzayuni huyo alisema: Hakuna mtu anayetutaka hapa, Waarabu wengi wanatuchukia.
Aidha alisema: Nina hakika viongozi wa Israel wanalijua hili na wanajua vizuri kwamba hawawezi kupata uhalali kwenye vikao vinavyofanya kwenye mahoteli na vituo vya maamuzi. Wananchi wa nchi za Kiarabu wana maoni tofauti. Israel haukubaliki na wanawahesabu wanafanya mapatano na Israel ni wasaliti.
Ikumbukwe kuwa, nchi za Kiarabu za mwisho kutangaza uhusiano wa kawaida na Wazayuni makatili ni Imarati, Bahrain, Sudan na Morocco. Kabla ya hapo utawala wa Kizayuni ulikuwa na uhusiano wa kawaida na nchi za Kiarabu za Jordan na Misri.
Hata hivyo uhusiano wa utawala wa Kizayuni na Jordan na Misri ni baridi sana kiasi kwamba, hata baada ya kupita miaka 40 ya uhusiano baina ya utawala wa Kizayuni na Misri, hakuna Mmisri hata mmoja anayeweza kuingia “Israel”, na yeyote anayefanya hivyo, Wamisri wanamtazama kuwa ni mamluki na msaliti. Hali ni hiyo hiyo huko Jordan.