Huku walowezi wa Kizayuni wakiendeleza hujuma zao dhidi ya raia wa Palestina, waliyateketeza kwa moto magari kadhaa ya Wapalestina katika mkoa wa Quds unaokaliwa kwa mabavu.
Mapema ya Ijumaa hii walowezi wa Kizayuni walichoma moto magari kadhaa ya Wapalestina katika vijiji viwili vya Abu Ghosh na Ain Naquba katika mkoa wa Quds unaokaliwa kwa mabavu.
Kwa mujibu wa ripoti ya tovuti ya “Palestine Ilyum”, duru za ndani zilisema kuwa walowezi wa Kizayuni walichoma moto magari manne katika eneo la Abu Ghosh, lililoko kaskazini magharibi mwa Quds inayokaliwa kwa mabavu na magari mengine manne huko Ain Naquba, magharibi mwa mji huo.
Aidha walowezi hao waliandika maneno ya ubaguzi wa rangi kwenye kuta za nyumba za Wapalestina katika vijiji hivi viwili.