Onyo kali la Yemen kwa muungano wa Saudia kuhusu kuendelea kuporwa nishati ya nchi hiyo

Huku uporaji wa mafuta ya Yemen ukiwa unaendelea, Abdul Aziz bin Habtour, Waziri Mkuu wa Serikali ya Wokovu wa Kitaifa ya Yemen ametahadharisha kuwa, iwapo uporaji huo utaendelea, Wayemen watalazimika kuzilenga meli za mafuta za muungano wa Saudia.

Vikosi vya jeshi la Yemen siku ya Jumatatu viliilazimisha meli ya mafuta iliyokuwa inapanga kukaribia bandari ya al-Dabbah, iliyoko mashariki mwa mji wa Makla, mji mkuu wa mkoa wa Hadhramaut (mashariki mwa Yemen), kuondoka kwenye bandari hiyo. Bandari hiyo inakaliwa na mamluki wa muungano vamizi wa Saudia na Imarati. Meli hiyo ilikuwa inapanga kupora mapipa milioni mbili ya mafuta ya Yemen.

Yemen ni mojawapo ya nchi maskini zaidi katika ulimwengu wa Kiarabu. Hali ya umaskini na njaa nchini humo imezidi kuwa mbaya katika kipindi cha miaka 8 iliyopita wakati muungano wa Saudia unaendeleza vita vya kichokozi dhidi ya nchi hiyo. Mbali na  muungano huo kufanya uharibifu mkubwa huko Yemen kutokana na mashambulio yake ya kijeshi ambapo raia wengi wa nchi hiyo wameuawa na mamilioni ya wengine kulazimika kuishi kama wakimbizi kwenye nchi yao wenyewe, muungano huo ungali unaisababishia nchi hiyo hasara kubwa ya kiuchumi kwa kuyakalia kwa mabavu maeneo ya mashariki na kusini mwa nchi kwa sababu rasilimali za nishati ya Yemen zinapatikana katika maeneo hayo.

Kwa kuzingatia muendelezo wa mchakato huo, Serikali ya Wokovu wa Kitaifa ya Yemen imeonya kwamba itachukua hatua za kijeshi dhidi ya meli za mafuta zinazopora mafuta ya nchi hiyo. Abd al-Aziz bin Habtour, Waziri Mkuu wa Serikali ya Wokovu wa Kitaifa ya Yemen, alisema Jumanne, akikusudia shambulio la tahadhari lililofanyika karibuni karibu na meli ya mafuta ya kigeni iliyokuwa ikijaribu kuiba mafuta ya Yemen kwamba: “Wakati ujao, hatutaionya meli yoyote, bali tutailenga moja kwa moja.” Bin Habtoor ameongeza kuwa: “Dunia nzima inapaswa kujua kwamba hatutaruhusu watu wetu wafe njaa ilihali muungano wa Saudia na Marekani wanapora utajiri wa Yemen.”

Ni wazi kwamba ikiwa muungano wa Saudia hautalichukulia kwa uzito onyo hilo la Waziri Mkuu wa Serikali ya Wokovu wa Kitaifa na kuendelea kupora rasilimali zake za nishati, vita vya Yemen vitaongezeka tena hivi karibuni.

Previous Post
Next Post

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *