Wanaakiolojia wa Jumba la Makumbusho la Akiolojia la London wametangaza kwamba utumwa umekuwepo nchini Uingereza tangu nyakati za Warumi.
Ni baada ya ripoti ya wanaakiolojia wa Jumba la Makumbusho la Akiolojia la London kuthibitisha kwamba, mifupa iliyopatikana katika eneo la Midlands Mashariki ya Uingereza ni ya mwanamume aliyekuwa na umri wa miaka 20 hadi 30 ambaye mikono na miguu yake ilikuwa katika pingu za chuma.
Huu ni ushahidi wa kwanza kuhusu historia ya utumwa nchini Uingereza wakati wa Warumi, ambao unaonesha mwili wa mtumwa iliyeachwa kwenye shimo ili afiye humo.
Mifupa ya mtumwa huyo ilipatikana wakati wa operesheni ya ujenzi huko Rutland na baada ya uchambuzi wa kaboni ya mifupa, imebainika kuwa ni ya kipindi cha mwaka 226 hadi 427 Miladia (AD). Wakati huo Warumi walikuwa wakidhibiti nchi ya Uingereza.
Katika karne ya 18, Uingereza ilikuwa mfanyabiashara mkubwa zaidi wa watumwa duniani kwa kuwateka nyara watu huru, hasa kutoka Afrika Magharibi, na kuwasafirisha na baadaye kuwauza Amerika na Ulaya.
Nyaraka za Hifadhi ya Taifa ya Uingereza zinaonesha kuwa, kati ya 1640 na 1807, zaidi ya watumwa milioni tatu walisafirishwa na Waingereza kutoka barani Afrika na kuuzwa katika maeneo mengine ya dunia. Baadhi ya watumwa hao walikufa katika safari hiyo ndefu, na wengine wapatao milioni 2.7 waliuzwa huko walikopelekwa.
Kwa mujibu wa sheria za Uingereza, leseni za biashara ya watumwa zilitolewa na utawala wa kifalme wa nchi hiyo.
Katika ripoti ya mwaka wa 2013, ilitangazwa kuwa wajumbe waliohitimu wa Kamati ya Chumba cha Pamoja katika Chuo Kikuu cha Oxford walipiga kura kwamba picha ya Malkia wa Uingereza inapaswa kuondolewa eneo hilo kwa sababu ni ukumbusho wa historia ya ukoloni wa nchi hiyo katika maeneo mbalimbali ya dunia.
Harakati ya Kupinga Alama za Ubaguzi wa Kimbari ya Uingereza pia imetangaza kuwa masanamu 78 ya wamiliki wa watumwa na waungaji mkono utumwa katika nchi hiyo yanapaswa kuvunjwa na kuharibiwa.