Wapalestina pawatatu wakiwemo ndugu wawili wa kiume wauliwa shahidi Ukingo wa Magharibi

Wapalestina watatu wakiwemo ndugu wawili wa kiume Jawaad na Dhaafar Abdurrahman wameuawa shahidi asubuhi ya leo baada ya kupigwa risasi na askari katili wa utawala haramu wa Kizayuni wa Israel katika kijiji cha Kafr Ain kaskazini mwa Ramallah, Ukingo wa Magharibi Palestina inayokaliwa kwa mabavu.

Duru za Palestina zimeripoti kuwa Dhaafar Abdurrahman Rimawi mwenye umri wa miaka 21 ameuawa shahidi kwa kupigwa risasi na askari wa utawala ghasibu wa Israel huko Kafr Ain, dakika chache baada ya kuuawa shahidi kaka yake.
Kuhusiana na tukio hilo, Wizara ya Afya ya Palestina imeripoti kuwa: baada ya kuuawa shahidi Dhaafar Rimawi dakika chache baada ya kuuliwa shahidi kaka yake Jawaad, idadi ya Mashahidi wa tukio hilo imeongezeka na kufikia watatu.
Jana usiku, yalizuka mapigano makali kati ya Wapalestina na wavamizi wa Kizayuni katika kitongoji cha Beit Amr kilichoko kaskazini mwa mji wa al Khalil na baadhi ya maeneo mengine ya Ukingo wa Magharibi wa Mto Jordan.
Shirika la Hilali Nyekundu la Palestina limetangaza alfajiri ya leo kuwa, Wapalestina 22 wamejeruhiwa katika mapigano hayo na askari vamizi wa utawala haramu wa Kizayuni, na kwamba hali za baadhi ya majeruhi ni mbaya
Previous Post
Next Post

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *