Indonesia yakataa kumpokea mjumbe maalumu wa kutetea ubaradhuli wa Marekani

Marekani imelazimika kufuta safari ya mjumbe wake maalumu wa kutetea eti haki za mabaradhuli (LGBTQ) nchini Indonesia, baada ya nchi hiyo ya kusini mashariki mwa Asia kusema kuwa haitampokea afisa huyo wa Washington.

Baraza la Maulamaa la Indonesia jana Ijumaa lilitoa taarifa ya kupinga safari ya Jessica Stern, mjumbe maalumu wa Marekani katika masuala ya usenge, usagaji na watu wenye kubadilisha jinsia (LGBTQ) katika nchi hiyo yenye idadi kubwa zaidi ya Waislamu duniani.

Anwar Abbas, Naibu Mwenyekiti wa baraza hilo amesema katika taarifa kuwa, “Kama taifa la kidini la lenye ustaarabu, tunaambiwa tuwaheshimu wageni; lakini hatuwezi kuwakubali wageni ambao lengo lao la kuja hapa (Indonesia) ni kunajisi thamani tukufu za kidini na kiutamaduni za taifa letu.”

Mjumbe huyo maalumu wa Marekani wa kutetea vitendo hivyo vya ufuska alitazamiwa kwenda Indonesia wiki ijayo, kama sehemu ya safari yake ya kuzitembelea nchi za Asia Mashariki, lakini amelazimika kuifuta ziara hiyo baada ya viongozi wa Indonesia kusema kuwa haitamruhusu atie mguu kwenye ardhi ya nchi hiyo.

Balozi wa Marekani nchini Indonesia, Sung Kim amedai kuwa, anatumai nchi mbili hizo zitaendelea kufanya mazungumzo juu ya kuheshimiwa haki za mabaradhuli na kwamba, “baada ya mazungumzo ya pande mbili, tumeamua kufuta safari ya mjumbe maalumu Stern nchini Indonesia.”

Mapema mwaka huu, Makamu wa Rais wa Indonesia, Ma’ruf Amin alilihutubia kongamano la walimu Waislamu nchini humo na kueleza bayana kuwa, vitendo vya ushoga na ubaradhuli ni mwenendo unaokiuka mipaka na usiokubalika.

 

Previous Post
Next Post

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *