Bunge la Indonesia limo mbioni kupasisha sheria ya kutoa adhabu kwa wanaofanya zinaa nchini humo, hatua ambayo inalenga kukabiliana na vitendo vya uasherati.
Taarifa kutoka Indonesia zinasema, Bunge la nchi hiyo linatarajiwa kupitisha sheria ya uhalifu mwezi huu itakayowaadhibu watu wanaoshiriki ngono nje ya ndoa na kwamba, adhabu hiyo inaweza kufikia kifungo cha hadi mwaka mmoja jela.
Duru za karibu na Bunge la Indonesia zinasema, huenda sheria hiyo ikapasishwa wiki ijayo.
Iwapo sheria hiyo itapitishwa, itawaadhibu raia wa Indonesia pamoja na raia wa kigeni ambao watapatikana na hatia ya kuzini na kushiriki tendo la ndoa nje ya ndoa.
Hata hivyo inaelezwa kuwa, adhabu hiyo ya uzinifu inaweza kutekelezwa tu iwapo watajitokeza watu na kuwasilisha malalamiko kwa mamlaka husika.
Kwa wale ambao wameoana, mmoja wao ana haki ya kuwasilisha malalamiko kama mshitakiwa ni mume au mke.
Sheria hiyo pia inawaruhusu wazazi wa watu ambao hawajaolewa kuwaripoti kwa kufanya ngono.
Aidha kwa wale ambao wameoana, mmoja wao ana haki ya kuwasilisha malalamiko kama mshtakiwa ni mume au mke.
Sheria hiyo pia inawaruhusu wazazi wa watu ambao hawajaolewa kuwaripoti kwa kufanya uzinzi.
Katika upande mwingine sheria hiyo kama itapasishwa itapiga marufuku pia kuishi pamoja mwanamke na mwanaume kabla ya ndoa na kwamba, wale watakaopatikana na hatia wanaweza kukabiliwa na hukumu ya kifungo cha miezi sita jela.