‘Arin al Usud: Tumefanya operesheni 5 za kulipiza kisasi dhidi ya Wazayuni

Kundi la mapambano ya Kiislamu la ‘Arin al Usud (Pango la Simba) linaloendesha mapambano yake katika Ukingo wa Magharibi wa Mto Jordan huko Palestina limetoa taarifa na kusisitiza kuwa limefanya operesheni tano za kulipizia kisasi cha kuuliwa shahidi na kikatili kijana wa Kipalestina, Ammar Mefleh.

Taarifa ya kundi hilo la muqawama wa Kiislamu imesema kuwa, operesheni hizo zimefanyika katika maeneo tofauti ya Nablos ikiwa ni pamoja na eneo aliouliwa kikatili kijana huyo wa Kipalestina na pia katika maeneo ya Beit Furik na Jarzim katika Ukingo wa Magharibi wa Mto Jordan.

Wakati huo huo duru za utawala wa Kizayuni zimekiri kwamba usiku wa kuamkia leo Jumanne, wanamapambano wa Palestina walifanya opereseheni ya ufyatuaji risasi dhidi ya mlowezi wa Kizayuni katika Ukingo wa Magharibi wa Mto Jordan.

Vyombo vya habari vya utawala wa Kizayuni leo Jumanne vimekiri kuwa, operesheni hiyo imefanyika karibu na Ramadhallah. Duru hizo za Kizayuni zimedai kuwa operesheni hiyo haikusababisha madhara makubwa.

Kukiri vyombo hivyo vya Kizayuni kumekuja huku kundi jipya la muqawama wa Palesina linalojulikana kwa jina la Baha Abul ‘Ataa likitangaza kuundwa kwake na kuanzisha opereseheni dhidi ya Wazayuni katika maeneo ya kusini magharibi mwa ardhi za Palestina zinazokaliwa kwa mabavu na Wazayuni.

Kundi hilo jipya la muqawama wa Palestina limesisitiza katika taarifa yake hiyo kwamba, wanamapambano wa Palestina wamerejea salama kwenye vituo vyao katika kitongoji cha Salim baada ya kuendesha kwa mafanikio opereseheni hiyo karibu na Ramadhallah.

Previous Post
Next Post

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *