Kukiri Marekani na Israel kuhusu kutotetereshwa Iran na machafuko ya hivi karibuni

Sambamba na himaya na uungaji mkono wa Marekani kwa wafanya fujo na machafuko nchini Iran, wachambuzi waandamizi wa masuala ya usalama wa Marekani na utawala haramu wa Israel wamekiri kwamba, Iran haijatetereshwa na machafuko hayo ya hivi karibuni.

Avril Haines, Mkurugenzi wa Ujasusi wa Kitaifa wa Marekani sanjari na kuashiria vurugu na machafuko ya Iran anaamini kuwa, machafuko hayo si tishio kwa mfumo wa Jamhuri ya Kiislamu. Brigedia Jenerali, Amit Saar mweledi mwandamizi wa masuala ya kjasusi katika jeshi la utawala ghasibu wa Israel amekiri kwamba, machafukko ya hivi karibuni nchini Iran hayawezi kuwa tishio kwa uwepo wa mfumo unaotawala nchini Iran.

Matamshi ya maafisa wa ngazi za juu wa masuala ya kiintelijensi wa Marekani na utawala haramu wa Israel ya kukiri kuhusu kutokuwa tishio machafuko ya Iran kwa mfumo unaotawala hapa nchini yanatokana na kuwa, mfumo unaotawala hapa nchini una ridhaa ya wananchi na hilo limeonekana wazi kupitia himaya na uungaji mkono wao kwa mfumo huu katika kipindi chote cha miongo minne iliyopita. Katika kipindi hicho, mfumo wa Jamhuri ya Kiislamu umeandamwa kwa njama mbalimbali lakini umezishinda njama hizo kwa himaya ya wananchi na kusimama kidete wananchi wa taifa hili katika kuutetea mfumo huu.

Machafuko ya mara hii yaliyoibuka kwa kisingizio cha kifo cha Mahsa Amini yalitazamwa na maadui wa mfumo huu kutoka nje kama fursa ya kuingilia masuala ya ndani ya Iran na kuchochea vurugu kadiri inavyowezekana ili kulitumbukiza taifa hili katika lindi la vurugu na machafuko na hatimaye kuuangusha mfumo wa Kiislamu unaotawala hapa nchini Iran.

Ukweli wa mambo ni kuwa, viongozi wa kisiasa wa Marekani, Ulaya, utawala wa Kizayuni wa Israel pamoja na vyombo vyao vya habari na vyombo vya habari vya lugha ya Kifarsi vyenye uadui sugu na mfumo wa Kiislamu na vinavyoungwa mkono na madola ya Magharibi kama Kanali ya Televisheni ya Iran International walilitumia vibaya tukio chungu la kifo cha Mahsa Amini ambapo wakitumia nara ya kuunga mkono haki za wananchi wa Iran walijitokeza na kuunga mkono watu wanaofanya fujo na kuharibu mali za umma na za watu.

Unafiki wa madola ya Magharibi ulionekana wazi pale walipoamua kufumbia macho au kuyadogosha maandamano makubwa ya wananchi wa Iran ya kuunga mkono mfumo wa Kiislamu na kutangaza kupinga vurugu na machafuko yanayowafanywa na baadhi ya watu wachache. Marekani ambayo imekuwa mstari wa mbele kuwaunga mkono wahuni na wafanya vurugu na machafukko hapa Iran ilitoa ahadi ya kuondoa vikwazo vya Internet sambamba na kuchukua misimamo ya kuingilia masuala ya ndani ya Iran ili kuchochea moto wa vurugu hizo. Hata hivyo baada ya majuma kadhaa, Marekani na washirika wake wamegonga mwamba na kushindwa kufikia malengo yao.

Katika hatua iliyofuata serikali ya Washington iliamua kuziwekea vikwazo asasi na shakhisia kadhaa kwa kisingizio kwamba, walihusika katika kukabiliana na waandamanaji. Vikwazo hivyo ambavyo vimekwwa kwa kisingizio cha kuwaunga mkono wananchi wa Iran vinakizana kikamilifu na sheria za kimataifa na hati ya Umoja wa Mataifa. Aidha vikwazo hivyo ni ishara ya wazi ya utendaji mwingine wa kinafiki wa Washington kuhusiana na Iran.

Wizara ya Hazina ya Marekani imedai kuwa, vikwazo hivyo vipya ni ishara nyingine ya wazi ya kufungamana Washington na suala la kuunga mkono haki ya mkusanyiko wa amani. Misimamo hiyo ya Marekani inachukuliwa katika hali ambayo, kwa upande mmoja serikali ya Rais Joe Biden inadai kuamiliana kidiplomasia na Iran kuhusiana na kadhia ya makubaliano ya nyukklia ya JCPOA na hata kuna taarifa za pande mbili kubadilishana jumbe kwa njia isiyo ya moja kwa moja na hata kung’ang’ania kwakkwe kuweko mazungumzo ya ana kwa ana na Tehran, na kwa upande wa pili inaingilia masuala ya ndani ya Iran na kuwaunga mkono wafanya fujo na vurugu hapa nchini.

Katika hali ambayo Marekani inadai kuwa, inawaunga mkono wananchi wa Iran wanaofanya maandamano ya hivi karibuni, tukitupia jicho utendaji wa Washington kuhusiana na Iran katika miongo kadhaa ya hivi karibuni tunaona ishara za wazi za chuki na uhasama uliokubuhu wa Washington dhidi ya taifa hili la Kiislamu.

Katika kipindi cha mjiaka 40 iliyopita, Iran imekuwa chini ya mashinikizo na vikwazo vya Marekani. Vikwazo hivyo vilichukua mkondo mpana zaidi katika kipindi cha utawala wa Rais Donald Trump na baada ya Washington kujitoa katika makubaliano ya nyuklia ya JCPOA.

Ni baada ya hapo ambapo Marekani ilianza kutekeleza kile ilichokiita “mashinikizo ya kiwango cha juu kabisa” dhidi ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran. Washington iliwekea vikwazo vikali kabisa Tehran kwa matumaini kwamba, taifa hili litasalimu amri mbele ya matakwa haramu ya dola hilo la kibeberu. Hata hivyo kama ilivyokiri yenyewe serikali ya Biden ni kuwa, mipango yote hiyo dhidi ya Iran imefeli na kugonga mwamba.

Licha ya ukweli huo, lakini serikali ya Biden ambayo ni sawa na mfa maji ambaye haishi kutapata ingali inafuatilia siasa za vikwazo ambazo kimsingi zimefeli na kugonga mwamba.

Previous Post
Next Post

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *