Waziri wa Lebanon asusia jopokazi la Uholanzi kwa kuwemo humo Mzayuni

Waziri wa Utamaduni wa Lebanon ametangaza kuwa atajiondoa katika jopokazi la ushirikiano baina ya Lebanon na Uholanzi kutokana na kuwemo humo mkurugenzi wa makumbusho ya utawala wa Kizayuni.

Shirika la habari la IRNA limeripoti habari hiyo kumnukuu Mohammed Wassam Al-Mortaza, Waziri wa Utamaduni wa Lebanon, akisema hayo jana Jumanne kwamba Lebanon imetia saini makubaliano na Jumba la Makumbusho la Akiolojia la Uholanzi (RMO) huko Leiden, Uholanzi.

Waziri wa Utamaduni wa Lebanon ameeleza kuwa, ushirikiano na Uholanzi ulipelekea kufunguliwa maonyesho hayo kwa mujibu wa makubaliano ya pande hizo mbili, na kuongeza kuwa maandalizi ya maonyesho hayo yalifanyika baada ya kuhakikisha kuwa hakuna hata mmoja kati ya watu wanaoshiriki katika maonyesho hayo aliyesafiri kwenda Israel au kuwa na uraia wa utawala huo pandikizi, lakini baadaye imegundulika kuwa, mkurugenzi wa makumbusho wa utawala wa Kizayuni amealikwa kwenye maonyesho hayo, hivyo ameamua kuyasusia.

Taarifa hiyo imeongeza kuwa, mara tu baada ya Wizara ya Utamaduni ilipofahamishwa suala hili, iliwasiliana na mkurugenzi wa makumbusho ya RMO na kuelezea upinzani wake wa kushirikishwa mtu huyo.

Majibu ya mkurugenzi wa makumbusho hayo ya RMO yameshindwa kuikinaisha Wizara ya Utamaduni ya Lebanon, hivyo amewasiliana na balozi wa Lebanon nchini Uholanzi na kumjulisha msimamo wa Waziri wa Utamaduni kuhusu kupinga kwake hatua yoyote ya kuhalalisha uhusiano na utawala wa Kizayuni Israel.

Kuhalalisha uhusiano wa nchi za Kiarabu na Israeli ni moja ya mhimili muhimu wa mpango wa Amerika wa mpango wa karne. Sera hiyo ilifuatiliwa kwa nguvu zaidi baada ya Donald Trump kuingia madarakani huko Marekani.

Uwepo wa viongozi kama vile Mohammed bin Salman nchini Saudi Arabia, Mohammed bin Zayed huko Imarati na Sheikh Hamad bin Isa nchini Bahrain kumetoa msukumo wa kujaribu kuhalalisha uhusiano wa nchi za Kiarabu na Israel kuliko hilivyokuwa huko nyuma.

Previous Post
Next Post

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *