Kandanda: Croatia na Argentina zatinga nusu fainali ya Kombe la Dunia

Timu za taifa za soka za Croatia na Argentina zimetinga hatua ya nusu fainali ya michuano yasoka ya Kombe la Dunia inayoendelea nchini Qatar baada ya kuibuka na ushindi kwenye mechi mbili za kwanza za robo fainali.

Argentina imefanikiwa kusonga mbele kwenda hatua ya nusu fainali baada ya mchezo wa kukata na shoka dhidi ya Uholanzi uliolazimisha mshindi baina ya timu hizo mbili kupatikana kwa njia ya mikwaju ya penati.

Argentina iliilaza Uholanzi kwa peneti 4-3 baada ya dakika 90 za mchezo kumalizika kwa sare ya mabao 2-2 na nyingine 30 za nyongeza kufikia mwisho bila ya kupatikana mshindi.

Mlinda mlango wa Argentina Emiliano Martinez alikuwa shujaa wa mpambano huo baada ya kupangua mikwaju miwili ya mwanzo ya penalti huku Lautaro Martinez akitikisa nyavu kwa mkwaju wa mwisho wa penalti uliofungua milango ya Argentina kufuzu hatua ya nusu fainali.

 Brazil yafungashwa virago na Croatia

Wakati Argentina inasonga mbele, miamba mingine ya soka ya Amerika ya Kusini, timu ya taifa ya soka ya Brazil imeyaa mashiondano hayo ya Kombe la Dunia baada ya kupoteza mechi ya kwanza ya robo fainali dhidi ya timuu ngumu ya Croatia.

Mechi hiyo nayo iliamuliwa kwa mikwaju ya penalti. Croatia ilipata ushindi wa penalti 4-2 na kujiwekea nafasi kwenye hatua ya nusu fainali kwa mara ya pili mfululizo kwenye Kombe la Dunia. Sasa Croatia watakutana na wababe Argentina katika mechi ya nusu fainali inayotarajiwa kuwa na ushindani mkali hasa kutokana na kiwango cha kusakata kabumbu kilichoonyeshwa na vijana wa Croatia.

Michezo mingine miwili ya kuwania tiketi ya nusu fainali itasakatwa leo. Wawawkilishi pekee wa Afrika waliosalia katika mashindano hayo Morocco watakuwa kkatika pata shika nguo kuchanika wakati watakapokutana na tiimu ya soka ya taifa ya Ureno. Katika mechi nyingine ambayo wajuzi wa mambo wanasema ni fainali ya kabla ya wakati, Uingereza itakuwa msambweni wakati itakapopepetana na miamba ya soka Ufaransa. Washindi wa leo watakutana katika nusu fainali.

 

Previous Post
Next Post

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *