Maafisa wa Somalia wametangaza kuuawa kwa magaidi 15 wa Al-Shabaab wameuwa katika mji mkuu wa nchi hiyo Mogadishu.
Kwa mujibu wa Shirika la Habari la Mehr, kamanda wa jeshi la Somalia Adwai Youssef amesma vikosi vya usalama vya nchi hiyo vimefanikiwa kuwaua magaidi 14 waliokuwa na silaha katika eneo la Dabq Labi na wakamwangamiza gaidi mwingine katika eneo la Wabri mashariki mwa Mogadishu.
Kulingana na afisa huyo wa jeshi la Somalia, kinara mmoja al-Shabaab katika medani za mapigano ameuawa pia katika operesheni hiyo ya vikosi vya Somalia.
Kwa mujibu wa ripoti hiyo, vikosi vya usalama vimeshadidisha operesheni zao dhidi ya wanamgambo wa al-Shabaab mjini Mogadishu.
Hivi karibuni jeshi la Somalia lilitangaza kwamba magaidi wapatao 700 wa kundi la ukufurishaji la al-Shabaab waliuawa na mji muhimu wa Adan Yabal ulioko katikati mwa nchi hiyo pia ulikombolewa.
Al-Shabaab ni kundi la wabeba silaha lenye mfungamano na mtandao wa kigaidi wa Al-Qaeda na limefanya operesheni nyingi za kigaidi ambazo zimeua mamia ya watu barani Afrika.
Kundi hilo limeshambulia mara kwa mara wanajeshi wa serikali na vikosi vya kulinda amani vya Umoja wa Afrika huko Mogadishu, mji mkuu wa Somalia, na limefanya operesheni kadhaa za umwagaji damu katika maeneo mengine ya Afrika.