Matokeo ya uchunguzi wa maoni uliofanyika Palestina yanaashiria kuenea kwa ufisadi ndani ya Mamlaka ya Ndani ya Palestina, kupungua sana umaarufu wa mamlaka hiyo na kupanda kwa nyota ya makundi ya wapiganaji wenye silaha kama Hamas na ‘Arin al Usud (Pango la Simba).
Matokeo ya uchunguzi huo ambao umefanywa na Kituo cha Utafiti wa Kisiasa na Maeneo cha Palestina kwa ushirikiano na Taasisi ya ” Konrad Adenauer” iliyopo mjini Ramallah, yanaonesha kuwa harakati ya Hamas inastahiki zaidi kuwawakilisha na kuwaongoza wananchi wa Palestina kuliko Mamlaka ya Ndani ya Palestina.
Utafiti huo unaonesha kwamba watu wa Palestina wana imani kubwa na wapiganaji wa makundi ya mapambano katika Ukingo wa Magharibi, kama vile kikosi cha “Arin al-Asud”.
Utafiti huo pia unaonesha kuwa umaarufu wa Mamlaka ya Ndani ya Palestina na viongozi wake (Mahmoud Abbas n.k.) umepungua, na upinzani wa kile kinachoitwa utatuzi wa serikali mbili (nchi mbili) na nchi moja umeongezeka, na kwamba watu wa Palestina wanataka serikali ya kidemokrasia.
Kinachodhihirika katika utafiti huo ni kwamba robo tatu ya wananchi wa Palestina wanamtaka Mahmoud Abbas ajiuzulu, na asilimia 69 ya wananchi wa Palestina wanataka kufanyanyike uchaguzi mkuu na wa kisheria mapema.
Wakati huo huo, asilimia 70 ya wananchi wamepongeza wazo la kuundwa makundi ya mapambano ya silaha kama vile “Arin al-Asud” ambavyo havitii amri za Mamlaka ya Ndani ya Palestina na si sehemu ya vikosi vya usalama.
Idadi kubwa ya watu wa Palestina (asilimia 87) pia wanasema kuwa Mamlaka ya Ndani ya Palestina haina haki ya kuwakamata wanachama wa harakati za mapambano katika Ukingo wa Magharibi; kwa sababu kukamatwa huko ni kwa ajili ya kuzuia operesheni za silaha dhidi ya utawala wa Kizayuni na kuunga mkono.