Uturuki yawatia nguvuni makumi ya majasusi wa Mossad

Vyombo vya habari vya Uturuki viliripoti leo, Jumatano, kwamba taasisi za usalama za nchi hiyo zimewakamata watu 44 wanaofanya kazi kwa maslahi ya shirika la ujasusi la Israeli (MOSSAD).

Gazeti la Uturuki “Sabah” limeripoti kwamba washukiwa hao wamekamatwa katika operesheni ya idara ya ujasusi ya Uturuki kwa ushirikiano na polisi wa Istanbul na Kitengo cha Kupambana na Ugaidi, baada ya kubainika kuwa baadhi makampuni ya usalama ya kibinafsi mjini Istanbul yanafanyia kazi shirika la ujasusi la Israel, Mossad, kuvujisha taarifa kuhusu Wapalestina na mashirika yasiyo ya kiserikali ya Palestina nchini Uturuki, mkabala wa kupewa fedha.

Gazeti hilo limeongeza kuwa mamlaka ya usalama bado inawasaka washukiwa wengine 13 ambao amekimbia.

Ripoti zinasema, washukiwa 7 kati ya yao wamefikishwa mahakamani, 7 wanashikiliwa mahabusu na wengine wanaendelea kuhojiwa na Kitengo cha Kupambana na Ugaidi cha Kurugenzi ya Usalama ya Istanbul.

Shirika la ujasusi la Israel, MOSSD, limekuwa likitumia wafanyabiashara, wanafunzi na makampuni ya usalama ya watu binafsi kufanya ujasusi katika nchi mbalimbali.

Mapema mwezi huu Iran iliwanyonga wahalifu wanne waliopatikana na hatia ya kushirikiana na shirika la ujasusi la Israel.

Mwezi Machi mwaka huu pia Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu nchini Iran (Sepah) lilishambulia kituo cha kutoa mafunzo za Shirika la Ujasusi la Israel (MOSSAD) kwa makombora ya balestiki katika eneo la Erbil, kaskazini mwa Iraq.

Maafisa wa ujasusi waliokuwa katika kituo hicho walingamizwa.

Previous Post
Next Post

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *