Watu 44 wakamatwa nchini Uturuki kwa tuhuma za kushirikiana na Mossad

Mamlaka ya usalama ya Uturuki iliwakamata watu 44 mjini Istanbul kwa madai ya ushirikiano na shirika la kijasusi la Kizayuni (Mossad).

Kwa mujibu wa ripoti ya Shirika la Habari la Fars, vyombo vya habari vya Uturuki vimefichua kuwa mamlaka ya usalama ya nchi hiyo imewakamata watu 44 mjini Istanbul kwa madai ya kushirikiana na shirika la kijasusi la Mossad.

Kwa mujibu wa habari,mamlaka ya Ankara iliendesha operesheni za usalama kwa lengo la kuwakamata “wapelelezi binafsi” waliokuwa wakifanya ujasusi wa Mossad, kufuatilia na kuwasaka watu wa Palestina na mashirika yasiyo ya kiserikali nchini Uturuki.

Previous Post
Next Post

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *