Israel kushirikiana na nchi tatu za Kiarabu katika kuunda “Mtambo wa Kuba la Chuma la Mtandao”

Utawala haramu wa Kizayuni wa Israel na nchi tatu za Kiarabu za Muungano wa Falme za Kiarabu (UAE), Bahrain na Morocco, zinapanga kuzindua mradi wa ulinzi wa anga unaoitwa Mtambo wa Kuba la Chuma la Mtandao, (Cyber ​​​​Iron Dome).

Vyombo vya habari vya Kizayuni vimetangaza kuwa maafisa wa utawala haramu wa Israel wamekutana na kufanya mazungumzo na viongozi wa Bahrain, Imarati na Morocco kujadili mpango wa kuunda mfumo wa pamoja wa ulinzi wa mtandao ili kukabiliana na kile kinachodaiwa kuwa ni “vitisho vya Iran”.
Gabi Portnoy, mkuu wa Shirika la Intaneti la Israel, ameiambia tovuti ya i24news: “huu ulikuwa mkutano wa kihistoria na pande zote zimetangaza utayari wao wa kushirikiana katika uga wa intaneti dhidi ya maadui zetu wa pamoja.”

Portnoy ameutaja mradi huo kwa jina la “Kuba la Chuma la Mtandao” akiunasibisha na mfumo wa ulinzi wa anga wa utawala wa Kizayuni wa Kuba la Chuma na kudai kwamba utawala huo umepiga hatua kubwa kimaendeleo katika uwanja wa mtandao wa intaneti.

Kwa mujibu wa Gabi Portnoy, mwishoni mwa mwezi uliopita wa Novemba, kulifanyika kongamano la kuonyesha teknolojia ya mtandao ya utawala wa Kizayuni kwa kushirikisha makampuni 65.
Vilevile, mwanzoni mwa mwezi huu wa Disemba, utawala wa Kizayuni wa Israel na Marekani zilifanya mazoezi ya pamoja ya mtandao ili kukabiliana na kile walichodai “vitisho vya kimtandao vya Iran”. Mazoezi hayo ambayo yalikuwa ya saba ya pamoja kati ya Washington na Tel Aviv katika uga wa mtandao yalifanyika kwa mara ya kwanza katika kituo cha mtandao cha Georgia kilichoko katika jimbo la Georgia nchini Marekani.
Previous Post
Next Post

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *