Wauguzi wagoma tena nchini Uingereza

Katika miezi kadhaa iliyopita, Uingereza imeshuhudia migomo mingi ya wafanyakazi wa sekta mbalimbali, ikiwa ni pamoja na sekta ya afya, sekta ya usafiri wa reli na wafanyakazi wa posta wanaolalamikia mishahara duni.

Kwa mujibu wa shirika la habari la Shirika la Utangazaji la Jamhuri ya Kiislamu ya Iran IRIB, wauguzi wa Uingereza waligoma jana Jumanne na kutishia kuendeleza mgomo huo hadi mishahara yao itakapoongezwa.

Wauguzi wa Uingereza pia waligoma Alhamisi iliyopita wakitaka nyongeza ya mishahara.

Mfumo wa afya huko Uingereza unafadhiliwa kwa kiasi kidogo sana. Mfumuko wa bei umefikia zaidi ya asilimia 10 na wauguzi wamekuwa alama ya taifa linalokumbwa na kupanda kwa gharama ya maisha na kuhisi kutoungwa mkono ipasavyo na serikali.

Mmoja wa wauguzi walioshiriki mgomo wa karibuni anasema: “Tunahitaji pesa na nguvukazi zaidi. Bima ya wagonjwa haitoshi. Tunafanya kazi nyingi na kulipwa mishahara duni.”

Kwa mujibu wa uchunguzi wa maoni uliochapishwa katika toleo la Jumapili iliyopita la gazeti la Sunday Times, karibu theluthi mbili ya raia wa Uingereza wanaunga mkono mgomo huo unaoendelea wa wauguzi.

Previous Post
Next Post

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *