Rais wa Chile, Gabriel Boric amesema nchi hiyo inapanga kufungua ubalozi wake huko Palestina kwa shabaha ya kuongeza kiwango cha uwakilishwaji wake rasmi katika taifa hilo linalokaliwa kwa mabavu na utawala wa Kizayuni wa Israel.
Chile ndiyo nchi yenye idadi kubwa ya Wapalestina nje ya eneo la Asia Magharibi, na tamko hilo la Rais Boric limetolewa wakati huu ambapo Benjamin Netanyahu, Waziri Mkuu wa utawala haramu wa Israel yupo mbioni kuunda baraza jipya la mawaziri la utawala huo pandikizi.
Rais Boric anatokea upande wa siasa za mrengo wa kushoto na anaiongoza Chile katika kipindi chake cha kwanza cha miaka minne madarakani kilichoanza mwezi Machi mwaka huu.
Mwaka 1998, Chile ilifungua ofisi yake ya ubalozi mjini Ramallah na mwaka 2011 iliitambua Palestina kama dola sanjari na kuunga mkono kupewa uanachama Palestina katika Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni UNESCO.
Si vibaya kuashiria hapa kuwa, Septemba mwaka huu, Rais wa Chile alikataa kupokea vitambulisho vya balozi mpya wa utawala wa Kizayuni wa Israel nchini humo, ikiwa ni kutangaza waziwazi uungaji mkono wake kwa wananchi wanaodhulumiwa wa Palestina.
Aidha Rais wa zamani wa Chile, Sebastián Piñera daima aliweka wazi msimamo wa nchi yake wa kuiunga mkono Palestina na kusisitiza kuwa, kuna haja ya kupewa uhuru taifa la Palestina.
Wazayuni waliingiwa na kiwewe rais huyo wa zamani wa Chile alipozuru Msikiti wa Al-Aqsa, kibla cha kwanza cha Waislamu akiandamana na maafisa na Idara ya Wakfu ya Kiislamu ya Quds na viongozi wa ngazi ya juu wa Mamlaka ya Ndani ya Palestina,