Utawala wa Kizayuni wazamisha Ukanda wa Gaza Kwa kufungua njia za maji

Usiku wa kuamkia Jumamosi, utawala wa Kizayuni ulilowesha makumi ya nyumba na mamia ya hekta za ardhi ya kilimo katika eneo hilo kwa kufungua mifereji ya maji ya mvua nyuma ya ukanda wa mpaka ulioko mashariki mwa Ukanda wa Gaza.

Shirika la habari la Palestina la “Ma’an” liliripoti, likinukuu chanzo cha ndani: “Mafuriko yaliyosababishwa na mvua yalizikumba nyumba za baadhi ya vitongoji vya Gaza City na Deir Balah na maeneo ya al-Zawaidah, al-Brij na Al- Nusirat iliyoko katikati mwa Ukanda wa Gaza na maeneo ya mashariki mwa mji wa Khan Yunis.Kutokana na hayo, wakulima wengi walipata hasara kubwa kutokana na uharibifu wa ardhi ya kilimo.

Mamia ya Wapalestina katika Ukanda wa Gaza waliomba usaidizi jana usiku na kuonya kuhusu maafa ya kibinadamu na mazingira.

Kuhusiana na hilo, duru za kimatibabu za Palestina zimeripoti kifo cha mtu mmoja katika mji wa Deir al-Balah na kujeruhiwa baadhi ya Wapalestina kutokana na mvua kubwa inayoendelea kunyesha na kuharibika kwa paa la baadhi ya nyumba. Manispaa ya Ukanda wa Gaza pia ilitangaza hali ya hatari katika mji huo.

Previous Post
Next Post

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *