Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Iran amesema kuhusiana na sifa za shakhsia ya Shahidi Suleimani ya kwamba, sifa za shakhsia ya Shahidi Suleimani zingali zinaiongezea nguvu kambi ya Muqawama.
Nasser Kan’ani amesema hayo leo katika meza duara ya mjadala wa kitaalamu wa kuzungumzia namna ya kupambana na ugaidi na misimamo ya kufurutu ada katika eneo la Asia Magharibi iliyofanyika hapa Tehran ikiangazia hatua za Shahidi Qassem Soleimani.
Kan’ani amebainisha kuwa, shakhsia ya Shahidi Soleimani imepambika kwa sifa na kwa pande kadhaa; na kama alivyoeleza Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu katika miongozo yake, shakhsia yake ya sifa na pande kadhaa pamoja na njia yake ya fikra ni vitu vya kutafitiwa na kuhakikiwa.
Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje amesema, moja ya sifa za shakhsia ya Shahidi Soleimani ni uwezo wake katika nguvu za kitaifa na kimataifa katika kambi ya mapambano na muqawama, na akafafanua kuwa, pande kadhaa za shakhsia ya Shahidi Soleimani zingali zinaendelea kuiongezea nguvu kambi ya Muqawama, na kwa hakika Haj Qassem alikuwa shakhsia wa kimataifa wa kambi ya mapambano.
Kan’ani amebainisha kuwa, kwa mtazamo wa mahesabu ya adui, gharama ya kumuua Shahidi Soleimani ilikuwa ndogo kuliko kuvumilia shakhsia yake iliyokuwa ikijenga nguvu na uwezo; na ndio maana walichukua hatua ya kumuua.
Luteni Jenerali Qassem Soleimani, aliyekuwa kamanda wa Kikosi cha Quds cha Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu, aliuawa shahidi Januari 3, 2020 katika shambulio la anga lililofanywa na jeshi vamizi na la kigaidi la Marekani karibu na uwanja wa ndege wa Baghdad, akiwa pamoja na Abu Mahdi Al-Muhandis, Naibu Mkuu wa harakati ya kujitolea ya wananchi wa Iraq ya Al-Hashd al-Shaabi na wanamapambano wengine wanane, wakati alipoelekea Iraq kwa mwaliko rasmi wa viongozi wa nchi hiyo.