Rais Samia amlilia Pele, atuma salamu za pole Brazil

Rais Samia Suluhu Hassan wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ameungana wanasiasa na wanasoka kote duniani kuomboleza kifo cha Pele.

Rais Samiai ametuma salamu za rambirambi kwa Rais wa Brazil, Jair Bolsonaro kufuatia kifo cha aliyekuwa mchezaji nguli wa mpira wa miguu wa nchi hiyo Edson Arantes do Nascimento ‘Pele’ aliyefariki jana akiwa na umri wa miaka 82.

Rais Samia kupitia mitandao yake ya kijamii aliandika”Nimepokea kwa masikitiko taarifa za kifo cha Mwanasoka wa Karne kutoka Brazil, Edson Arantes do Nascimento “Pelé”.

Mchango wake katika soka duniani utakumbukwa daima. Pole kwa Rais wa Brazilfamilia & mashabiki wote wa soka. Mungu amweke mahali pema peponi, amina,” ameandika Rais Samia.

Rais Samia anaungana na wanasiasa wengine duniani akiwamo Rais wa Kenya, William Ruto na Rais wa Marekani, Joe Biden, wanasoka na wapenzi wa soka kuomboleza kifo cha gwiji huyo.

Nguli huyo wa soka alitumia muda mwingi alipostaafu kusaidia Umoja wa Mataifa na kazi zake, kama balozi wa mwema wa shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto UNICEF, na kama bingwa wa UNESCO wa michezo, kutoka mwaka 1994.

Pele pia aliteuliwa kuwa balozi mwema wa mkutano muhimu wa Umoja wa Mataifa wa dunia, huko Rio de Janeiro, mwaka 1992, moja ya mikutano mikuu ya kwanza ya maendeleo ya kimataifa na mazingira inayojikita na mustakabali endelevu zaidi kwa wote.

Previous Post
Next Post

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *